Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Unyenyekevu

Maisha na kazi

Biblia inasema nini kuhusu Unyenyekevu

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

2 Nya 7:14kisha watu wangu, ambao wameitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, kuomba, kuutafuta uso wangu, na kuziacha njia zao mbaya, nitasikia kutoka mbinguni, kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao.
1 Pet 5:6Kwa hiyo nyenyekeni chini ya mkono wa Mungu uliyo hodari ili kwamba awainue kwa wakati wake.
Yak 4:6Lakini Mungu hutoa neema zaidi, ndiyo maana maandiko husema, “Mungu humpinga mwenye kiburi, lakini humpa neema mnyenyekevu.”
Mit 22:4Thawabu ya unyenyekevu na kumcha Yehova ni utajiri, heshima na uzima.
Mit 11:2Kinapokuja kiburi, ndipo aibu huja, bali unyenyekevu huleta hekima.
Yak 4:10Jinyenyekezeni wenyewe mbele za Bwana, na atawainua juu.
Mik 6:8Amekwambia, mtu, kile kilicho bora, na kile ambacho Yahwe atakacho kutoka kwako: Kutenda haki, kupenda ukarimu, na kutembea kwa unyenyekevu pamoja na Mungu wako.
Efe 4:2Muishi kwa unyenyekevu mkuu na upole na uvumilivu. Mkichukuliana katika upendo.
1 Pet 5:5Vilevile, nanyi vijana wadogo, nyenyekeni kwa wakubwa wenu. Ninyi nyote, uvaeni unyenyekevu na kuhudumiana ninyi kwa ninyi, kwani Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa neema wanyenyekevu.
Kol 3:12Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0