Mwanzo › Biblia inasema nini › Haki
Maisha na kazi
Biblia inasema nini kuhusu Haki
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Mik 6:8
Amekwambia, mtu, kile kilicho bora, na kile ambacho Yahwe atakacho kutoka kwako: Kutenda haki, kupenda ukarimu, na kutembea kwa unyenyekevu pamoja na Mungu wako.Law 19:15
Usisababishe hukumu ikawa ya uongo. Usionyeshe upendeleo kwa mtu fulani eti kwa kuwa tu yeye ni masikini na usionyeshe upendeleo kwa mtu fulani eti kwa kuwa tu yeye ni mtu muhimu. Badala yake, amua juu ya jirani yako kwa haki.Kut 23:1–3
Haupaswi kutoa taarifa ya uongo kuhusu yeyote. usijiunge na mwanaume muovu kuwa shahidi wa uongo. Haupaswi kufuata umati kufanya uovu, wala kutoa ushahidi ukiwa na umati ili kupotosha haki. Haupaswi kumpendelea mwanaume maskini kwenye kesi yake.Kum 1:16–17
Niliwaamuru waamuzi wenu kwa wakati huo, kusema, 'Zikiliza mabishano kati ya ndugu zenu, na muhukumu ya haki kati ya ndugu na ndugu zake, na mgeni aliye pamoja naye. Hamtaonesha upendeleo kwa yeyote katika mgogoro, mtasikia madogo na makubwa pia. Hamtaogopa uso wa mtu, kwa kuwa hukumu ni ya Mungu. Migogoro iliyo migumu kwenu, mtaniletea mimi, na mimi nitaisikiliza.Isa 1:17
jifunze kutenda mema; tafuta ukweli; msiwanyanyase, wapeni haki yatima, walindeni wajane.''Amo 5:24
Badala yake, acheni haki itiririke kama maji, na haki kama mkondo utiririkao siku zote.Mit 21:15
Haki ikitendeka, huleta furaha kwa mwenye kutenda wema, lakini huleta hofu kubwa kwa watenda mabaya.Isa 30:18
Lakini Bwana anawasubiri ili awape neema yake, Hivyo basi yuko tayari kuwaonyesha huruma. Maana Yahwe na Mungu wa haki; Huwabarikiwe wale wanaomsubiri yeye.Zab 33:5
Yeye hupenda haki na kutenda kwa haki. Dunia imejaa uaminifu wa agano la Yahwe.Isa 61:8
Maana Mimi, Yahwe, ninapenda haki, na ninachukia wizi na vurugu zisizo za haki. Nitawalipa wao kataka haki na Nitafanya agano la milele na wao.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0