Mwanzo › Biblia inasema nini › Ukarimu
Maisha na kazi
Biblia inasema nini kuhusu Ukarimu
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (11), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Lk 6:38
Wapeni wengine, nanyi mtapewa. Kiasi cha ukarimu - kilichoshindiliwa, kusukwasukwa na kumwagika - kitamwagika magotini penu. Kwa sababu kwa kipimo chochote mnachotumia kupimia, kipimo hicho hicho kitatumika kuwapimia ninyi.”Mdo 20:35
Katika mambo yote niliwapa mfano wa jinsi inavyopasa kuwasaidia wanyonge kwa kufanya kazi, na jinsi mnavyopaswa kukumbuka maneno ya Bwana Yesu, maneno ambayo yeye mwenyewe alisema: “Ni heri kutoa kuliko kupokea.”2 Kor 9:7
Basi na kila mmoja atoe kama alivyopanga moyoni mwake. Basi naye asitoe kwa huzuni au kwa kulazimishwa. Kwa kuwa Mungu humpenda yule atoaye kwa furaha.Mit 11:24–25
Kuna yule ambaye hupanda mbegu- atakusanya zaidi; mwingine hapandi- huyo anakuwa masikini. Mtu mkarimu atafanikiwa na yule awapaye maji wengine atapata maji yake mwenyewe.Mit 19:17
Mwenye ukarimu kwa masikini humkopesha Yehova na atalipwa kwa kile alichofanya.2 Kor 9:6
Wazo ni hili: mtu apandaye haba pia atavuna haba, na yeyote apandaye kwa lengo la baraka pia atavuna baraka.1 Tim 6:17–19
Waambie matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, na wasitumaini katika utajiri, ambao siyo wa uhakika. Badala yake, wanapaswa kumtumaini Mungu. Ambaye hutupatia utajiri wote wa kweli ili tufurahie. Waambie watende mema, watajirike katika kazi njema, wawe wakarimu, na utayari wa kutoa. Katika njia hiyo watajiwekea msingi mzuri kwa mambo yajayo, ili kwamba waweze kushika maisha halisi.Ebr 13:16
Na usisahau kufanya mazuri na kusadiana ninyi kwa ninyi, kwa kuwa ni kwa sadaka kama hiyo ndiyo Mungu hupendezwa sana.1 Yoh 3:17
Lakini yeyote aliye na vitu, na anamuona ndugu yake mwenye uhitaji, lakini huuzuia moyo wake wa huruma kwa ajili yake; je, upendo wa Mungu unakaaje ndani yake?Mit 22:9
Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa, maana anashiriki mkate wake pamoja na masikini.Mit 3:27
Usizuie mema kwa wale wanaoyastahili, wakati utendaji upo ndani ya mamlaka yako.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0