Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Kutumia muda vizuri

Maisha na kazi

Biblia inasema nini kuhusu Kutumia muda vizuri

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Efe 5:16Ukomboeni muda kwa kuwa siku ni za uovu.
Zab 90:12Hivyo utufundishe sisi kuyafikiria maisha yetu ili kwamba tuweze kuishi kwa hekima.
Kol 4:5Enenda kwa hekima kwa wale walioko nje, na muukomboe wakati.
Yak 4:14Ni nani ajuaye nini kitatokea kesho, na maisha yenu ni nini hasa? Kwa kuwa mnafanana kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi na kisha hupotea.
Mhu 3:1Kwa kuwa kila kitu na wakati wake, na majira kwa kila kusudi chini ya mbingu.
Zab 31:15Hatima yangu iko mikononi mwako. Uniokoe mikononi mwa maadui zangu na wale wanao nifukuzia.
2 Pet 3:8Hii haiwezi kuchenga ujumbe wako, wapendwa, kwamba siku moja kwa bwana ni kama miaka elfu moja. Na miaka elfu moja ni kama siku moja.
Efe 5:15Hivyo iweni makini jinsi mtembeavyo, siyo kama watu wasio werevu bali kama werevu.
Mit 6:6–8Wewe mtu mvivu, mwangalie mchwa, zitafakari njia zake ili kupata busara. Hana akida, afisa au mtawala, lakini huandaa chakula chake wakati wa joto na wakati wa mavuno huweka hazina ili kula baadaye.
Lk 14:28Maana ni nani kati yenu, ambaye anatamani kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama kwa mahesabu kama ana kile anachohitaji ili kukamilisha hilo?

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0