Mwanzo › Biblia inasema nini › Afya
Maisha na kazi
Biblia inasema nini kuhusu Afya
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
1 Kor 6:19–20
Hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, yule ambaye mlipewa kutoka kwa Mungu? Hamjui kwamba si ninyi wenyewe? Kwamba mlinunuliwa kwa thamani. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu kwa miili yenu.3 Yoh 1:2
Mpendwa, nakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema, kama vile roho yako inavyofanikiwa.1 Kor 10:31
Kwa hiyo, chochote mnachokula au kunywa, au chochote mfanyacho, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.Mit 17:22
Moyo mchangamfu ni dawa njema, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.1 Tim 4:8
Kwa maana mazoezi ya mwili yafaa kidogo, bali utauwa wafaa sana kwa mambo yote. Hutunza ahadi kwa maisha ya sasa na yale yajayo.Kut 15:26
Alisema, “Kama utasikiliza sauti ya Yahweh Mungu wako kwa umakini, na kufanya yalio sahihi machoni pake, na kama utatega sikio kwa amri zake na kutii sheria zake zote - sitawaekea ninyi magonjwa yale niliyo waekea Wamisri, kwa kuwa mimi ni Yahweh ninaye kuponya.”Mit 3:7–8
Usiwe mwenye busara machoni pako mwenyewe; mche Yehova na jiepushe na uovu. Itakuponya mwili wako na kukuburudisha mwili wako.1 Kor 3:17
Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu yule. Kwa kuwa hekalu la Mungu ni takatifu, na hivyo na ninyi.Mit 16:24
Maneno yenye kufaa ni sega la asali -matamu kwenye nafsi na huponya mifupa.Mwa 1:29
Mungu akasema, “tazama, nimewapeni kila mmea uzaao mbegu ambao uko juu ya nchi, na kila mti wenye tunda ambalo lina mbegu ndani yake. Vitakuwa ni chakula kwenu.Mit 31:17
Yeye mwenyewe hujivika nguvu na kuimarisha mikono yake.Kut 23:25
Lazima umuabudu Yahweh Mungu wako, na atabariki mkate wako na maji. Nitaondoa magonjwa miongoni mwenu.Yer 33:6
Lakini ona, niko karibu kuleta uponyaji na tiba, kwa maana nitawaponya na nitawapa wingi wa, amani na uamainifu.Yak 5:15
na maombi ya imani yatamponya mgonjwa, na Bwana atamwinua. Na kama atakuwa ametenda dhambi, Mungu atamsamehe.Yak 5:16
Kwa hiyo ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana kila mmoja na mwenzake, ili muweze kuponywa. Maombi ya mwenye haki huzaa matokeo makubwa.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0