Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Pumziko na uchovu

Maisha na kazi

Biblia inasema nini kuhusu Pumziko na uchovu

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Mt 11:28–30Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
Isa 40:31Lakini wale watakao mngojea Yahwe watapewa nguvu mpya; na watapaa kwa mbawa kama malaika; watakimbia wala hawatachoka; watatembea wala hawatazimia.
Isa 40:29Anawapa nguvu waliochoka; na atawapa nguvu mpya waliowadhaifu.
Yer 31:25Kwa maana nitawapa majai ya kunywa waliochoaka, na nitamjaza kila anayeteseka na kiu.”
Zab 37:7Uwe kumya mbele za Yahwe na umsubiri yeye kwa uvumilivu. Usikasirike ikiwa kuna mtu anafanikiwa kwa kile afanyacho, au afanyapo njama za uovu.
Isa 40:28Je hakufahamu? Mungu wa milele, Yahwe, Muumbaji wa miisho ya nchi, apatwi na uchovu wala hachoki; hakuna mipaka katika ufahamu wake.
Zab 46:10Mkae kimya na mjue kuwa mimi ni Mungu; nitainuliwa juu ya nchi.
Ebr 4:9–11Kwa hiyo bado kuna Sabato ya pumziko iliyotunzwa kwa ajili ya watu wa Mungu. Kwani anayeingia katika pumziko la Mungu yeye mwenyewe pia amepumzika kutokana na matendo yake, kama Mungu alivyofanya katika yeye. Kwa hiyo tuweni na shauku ya kuingia katika lile pumziko, ili kwamba asiwepo atakayeanguka katika aina ya uasi waliofanya.
Mwa 2:2Siku ya saba Mungu alifikia mwisho wa kazi yake ambayo aliifanya, na kwa hiyo alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote.
Zab 4:8Ni amani kuwa nitajilaza na kusinzia, kwako pekee, Yahweh, nifanye kuwa salama kabisa.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0