Mwanzo › Biblia inasema nini › Tamaa
Maisha na kazi
Biblia inasema nini kuhusu Tamaa
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Ebr 13:5
Basi njia zenu za maisha ziwe huru katika upendo wa pesa. Muwe wanoridhika na vitu mulivyonavyo, kwani Mungu mwenyewe alisema, “Sitawaacha ninyi kamwe, wala kuwatelekeza ninyi.”1 Tim 6:10
Kwa kuwa kupenda fedha ni chanzo cha aina zote za uovu. Watu ambao hutamani hiyo, wamepotoshwa mbali na imani na wamejichoma wenyewe kwa huzuni nyingi.Mt 6:24
Hakuna hata mmoja anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali.Flp 2:4
Kila mmoja wenu asiangalie tu mahitaji yake binafsi, bali pia ajali mahitaji ya wengine.Lk 12:15
Ndipo akawaambia, Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo.”Mit 28:25
Mtu mwenye tamaa huchochea mafarakano, bali anayemtumaini Yehova atafanikiwa.1 Tim 6:9
Sasa hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu, katika mtego. Huanguka katika upumbavu mwingi na tamaa mbaya, na katika kitu chochote kinachowafanya watu wazame katika maangamizi na uharibifu.Mhu 5:10
Yeyote apendaye fedha hatatosheka na fedha, na yeyote apendaye utajiri mara zote hutaka zaidi. Huu pia ni mvuke.Mit 15:27
Mporaji huleta shida kwenye familia yake, bali yeye ambaye huchukia rushwa ataishi.Mit 11:24
Kuna yule ambaye hupanda mbegu- atakusanya zaidi; mwingine hapandi- huyo anakuwa masikini.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0