Mwanzo › Biblia inasema nini › Uvivu
Maisha na kazi
Biblia inasema nini kuhusu Uvivu
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Mit 10:4
Mkono mlegevu humfanya mtu awe masikini, bali mkono wa mtu mwenye bidii hupata utajiri.2 The 3:10
Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, “Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile.”Mit 6:9
Ewe mtu mvivu, utalala hata lini? Wakati gani utainuka usingizini?”Mit 13:4
Hamu ya watu wavivu ni uchu lakini hawapati kitu, bali hamu ya watu wenye bidii hutoshelezwa sana.Kol 3:23
Chochote mfanyacho, fanyeni kutoka nafsini mwenu kama kwa Bwana na si kama kwa wanadamu.Mit 20:4
Mtu mvivu halimi majira ya kipupwe; hutafuta mazao wakati wa mavuno lakini hapati kitu.Mit 6:6
Wewe mtu mvivu, mwangalie mchwa, zitafakari njia zake ili kupata busara.Mit 21:25
Shauku ya mtu mvivu itamuua, maana mikono yake hukataa kufanya kazi.Mit 18:9
Basi, ambaye ni mzembe katika kazi yake ni ndugu yake anayeharibu wengi.Mit 20:13
Usipende usingizi au utakuwa masikini; fumbua macho yako na utakuwa na vyakula tele.Mit 12:24
Mkono wa mwenye bidii utatawala, bali watu wavivu watawekwa katika kazi za kulazimishwa.Mit 14:23
Katika kazi zote ngumu huja faida, bali palipo na maongezi tu, huelekea kwenye umasikini.2 The 3:11–12
Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi wanaenenda kwa uvivu miongoni mwenu. Hawafanyi kazi lakini badala yake ni watu wasio na utaratibu. Sasa hao nao tunaagiza na kuwaasa katika Bwana Yesu Kristo, kwamba lazima wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.Mit 22:13
Mtu mvivu husema, “ Kuna simba mtaani! Nitauwawa sehemu za njia.”Mit 19:15
Uvivu unamtupa mtu kwenye usingizi mzito, bali asiyetamani kufanya kazi atakwenda njaa.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0