Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Usingizi

Maisha na kazi

Biblia inasema nini kuhusu Usingizi

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (11), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Zab 4:8Ni amani kuwa nitajilaza na kusinzia, kwako pekee, Yahweh, nifanye kuwa salama kabisa.
Mit 3:24ulalapo hutaogopa; utakapolala, usingizi wako utakuwa mtamu.
Zab 127:2Ni kazi bure kwa wewe unayeamka mapema, na kulala kwa kuchelewa, au kula mkate kwa kuufanyia kazi ngumu, maana Yahwe huwapa chakula awapendao hata wawapo usingizini.
Zab 91:5Nawe hautaogopeshwa na vitisho wakati wa usiku, wala mishale ipaayo kwa siku,
Mt 11:28Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha.
Mit 20:13Usipende usingizi au utakuwa masikini; fumbua macho yako na utakuwa na vyakula tele.
Zab 3:5Nilijilaza chini na kusinzia; na niliamka, kwa kuwa Yahweh alinilinda.
Mt 8:24Tazama, ikainuka dhoruba kuu juu ya bahari, kiasi kwamba mtumbwi ulifunikwa na mawimbi. Lakini Yesu alikuwa amelala.
Zab 121:3–4Hatauacha mguu wako uteleze; yeye akulindaye hatasinzia. Tazama, mlinzi wa Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi kamwe.
Mit 19:23Kumheshimu Yehova huwaelekeza watu kwenye uzima; mwenye nayo atashibishwa na hatadhurika kwa madhara.
Mit 6:22utembeapo, yatakuongoza; ulalapo yatakulinda, na uamkapo yatakufundisha.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0