Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Kufanya maamuzi

Maisha na kazi

Biblia inasema nini kuhusu Kufanya maamuzi

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Mit 3:5–6Mtegemee Yehova kwa moyo wako wote na wala usitegemee ufahamu wako mwenyewe, katika njia zako zote mkiri Yeye na yeye atayanyosha mapito yako.
Yak 1:5Lakini kama mtu kati yenu anahitaji hekima, aiombe kutoka kwa Mungu, ambaye hutoa kwa ukarimu na pasipo kukemea kwa wote wamwombao, na atawapa hekima.
Mit 11:14Pasipokuwa na uongozi wenye busara, taifa huanguka, bali ushindi huja kwa kushauriana washauri wengi.
Flp 4:6–7Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali, kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu. Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaad Kristo Yesu.
Mit 12:15Njia ya mpumbavu ni sawa machoni pake mwenyewe, bali mtu wa hekima husikiliza ushauri.
Mit 15:22Mipango huharibika ambapo hakuna ushauri, bali washauri wengi wanafanikiwa.
Isa 30:21Masikio yako yatasikia maneno yanayosemwa nyuma, Hii ndio njia, pitia hii, ''utakapogeuka upande wa kulia au utakageuka upande wa kushoto.
Zab 32:8Nitakuelekeza na kukufundisha katika njia upasayo kuiendea. Nitakuelekeza huku macho yangu yakikutazama.
Mit 18:15Moyo wa mwenye akili hujipatia maarifa na usikivu wa mwenye busara huitafuta.
Mit 16:9Katika moyo wake mtu hunuia njia yake, bali Yehova huziongoza hatua zake.
Rum 12:2Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Fanyeni hivi mpate kujua mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yakumpendeza na kamilifu.
Mit 2:6Kwa kuwa Yohova hutoa hekima, katika kinywa chake hutoka maarifa na ufahamu.
1 Fal 3:9Kwa hiyo umpe mtumishi wako moyo wa uelewa wa kuwahukumu watu wako. Kwani ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?”
Mit 16:3Kabidhi kwa Yehova kazi zako zote na mipango yako itafanikiwa.
Mit 1:5Watu wenye busara wasikie na kuongeza elimu yao na watu wenye ufahamu wapate mwongozo,

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0