Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Hekima

Maisha na kazi

Biblia inasema nini kuhusu Hekima

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Yak 1:5Lakini kama mtu kati yenu anahitaji hekima, aiombe kutoka kwa Mungu, ambaye hutoa kwa ukarimu na pasipo kukemea kwa wote wamwombao, na atawapa hekima.
Mit 1:7Hofu ya Yehova ni chanzo cha maarifa- wapumbavu hudharau hekima na nidhamu.
Yak 3:17Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, kisha kupenda amani, upole na ukarimu, yenye kujaa rehema na matunda mema, bila kupendelea watu fulani, na kweli.
Efe 5:15Hivyo iweni makini jinsi mtembeavyo, siyo kama watu wasio werevu bali kama werevu.
Mit 2:6Kwa kuwa Yohova hutoa hekima, katika kinywa chake hutoka maarifa na ufahamu.
Mt 10:16Angalia, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu, kwa hiyo iweni na werevu kama nyoka na wapole kama njiwa.
Yak 3:13–14Ni nani miongoni mwenu aliye na hekima na ufahamu? Hebu mtu huyo na aoneshe maisha mema katika kazi zake kwa unyenyekevu utokanao na hekima. Lakini kama mnao wivu mkali na nia ya ubinafsi mioyoni mwenu, msijivune na kusema uongo mkiupinga ukweli.
Zab 111:10Kumcha Yahwe ni mwanzo wa hekima; wale washikao maagizo yake wana uelewa mzuri. Sifa yake yadumu milele.
Mhu 7:12Kwa kuwa hekima hutoa ulinzi kama vile fedha inavyoweza kutoa ulinzi, lakini faida ya maarifa ni kwamba hekima humpa uhai kwa yeyote aliye nayo.
Mit 19:20Sikiliza ushauri na ukubali maelekezo, ili uweze kuwa na hekima mwishoni mwa maisha yako.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0