Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Kujitawala

Maisha na kazi

Biblia inasema nini kuhusu Kujitawala

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Mit 25:28Mtu bila kujitawala ni kama mji ulibomolewa na usiokuwa na kuta.
Gal 5:22–23Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani, upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo.
2 Tim 1:7Kwa kuwa Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na upendo na nidhamu.
1 Kor 10:13Hakuna jaribu lililowapata ninyi lisilo kawaida ya wanadamu. Ila Mungu ni mwaminifu. Hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu. Pamoja na jaribu yeye atawapa mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
Mit 16:32Ni bora kukawia kuwa na hasira kuliko kuwa shujaa na mwenye kutawala roho yake ni imara zaidi kuliko yule anayeuteka mji.
2 Pet 1:5–6Kwa sababu hii, fanyeni bidii kuongeza uzuri kwa njia ya imani yenu, kwa sababu ya uzuri, maarifa. Kupitia maarifa, kiasi, na kupitia kiasi saburi, na kupitia saburi, utauwa.
1 Pet 4:7Mwisho wa mambo yote unakuja. Kwa hiyo, mwe na ufahamu ulio sahihi, na iweni na nia njema kwa ajili ya maombi yenu.
1 Kor 9:27Lakini nautesa mwili wangu na kuufanya kama mtumwa, ili kwamba nijapokwisha kuwahubiri wengine, mimi mwenyewe nisiwe wa kukataliwa.
1 Pet 5:8Iweni na busara, iweni waangalifu. Yule adui yenu, ibilisi, kama simba aungurumaye ananyatia, akisaka mtu wa kumrarua.
Mit 29:11Mpumabavu huonyesha hasira yake, bali mtu mwenye busara huishikilia na kujituliza mwenyewe.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0