Mwanzo › Biblia inasema nini › Kuwasaidia maskini
Maisha na kazi
Biblia inasema nini kuhusu Kuwasaidia maskini
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Mit 19:17
Mwenye ukarimu kwa masikini humkopesha Yehova na atalipwa kwa kile alichofanya.Mit 14:31
Anayemkandamiza masikini humlaani Muumba wake, bali anayeonyesha fadhila kwa wahitaji humtukuza yeye.1 Yoh 3:17–18
Lakini yeyote aliye na vitu, na anamuona ndugu yake mwenye uhitaji, lakini huuzuia moyo wake wa huruma kwa ajili yake; je, upendo wa Mungu unakaaje ndani yake? Watoto wangu wapenzi, tusipende kwa midomo wala kwa maneno matupu bali katika vitendo na kweli.Gal 2:10
Pia walitutaka sisi kuwakumbuka masikini. Mimi pia nilikuwa natamani kufanya jambo hili.Mit 28:27
Mwenye kuwapa masikini hatapungukiwa kitu, bali anayewafumbia macho atapokea laana nyingi.Mit 22:9
Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa, maana anashiriki mkate wake pamoja na masikini.Law 25:35
Ikiwa mwananchi mwenzako anakuwa masikini, kiasi kwamba hawezi kujihudumia, nawe utalazimika kumsaidia kama vile ungemsaidia mgeni au mwingine yeyote kutoka nje aishie miongoni mwenu.Lk 14:12–14
Yesu pia alimwambia mtu aliyemwalika, 'Unapotoa chakula cha mchana au cha jioni, usiwaalike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako matajiri, ili kwamba wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Badala yake, unapofanya sherehe, waalike maskini, vilema, viwete na vipofu, na wewe utabarikiwa, kwa sababu hawawezi kukulipa. Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.”Mit 31:8–9
Ongea kwa ajili yao wasioweza kuongea, kwa madai ya wote wanaopotea. Ongea na uhukumu kwa vipimo vya haki na utetee dai la masikini na watu wahitaji.Mdo 20:35
Katika mambo yote niliwapa mfano wa jinsi inavyopasa kuwasaidia wanyonge kwa kufanya kazi, na jinsi mnavyopaswa kukumbuka maneno ya Bwana Yesu, maneno ambayo yeye mwenyewe alisema: “Ni heri kutoa kuliko kupokea.”Mt 19:21
“Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze ulivyo navyo, na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo unifuate.”Mit 14:21
Yeye ambaye huonyesha dharau kwa jirani yake anafanya dhambi, bali yule ambaye huonyesha fadhila kwa masikini anafuraha.Mit 29:7
Atendaye haki hutetea madai ya masikini; mtu mwovu hafahamu maarifa kama hayo.Yak 2:15–16
Kama ndugu wa kiume au wa kike ni muhitaji wa mavazi au chakula cha kila siku, na mmoja wenu akawaambia, “Nendeni kwa amani, mkaote moto na mle vizuri,” lakini hamuwapi mahitaji muhimu ya mwili, hiyo yafaaa nini?Isa 58:6–7
Hii sio mfungo ambao niliuchagua mimi: kufungua vifungo vya waovu, kufungua kamba za nira, kuwaweka huru walioangamizwa, na kuharibu kila nira? Sio kwamba kula mkate na wenye njaa na kuwaleta masikini na kuwaleta wasio na makazi katika nyuma yako?'' Unapomuana mtu yuko uchi, unatakiwa vumvishe mavazi; na usijifiche mwenyewe na ndugu zako.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0