Mwanzo › Biblia inasema nini › Maneno na usemi
Mahusiano
Biblia inasema nini kuhusu Maneno na usemi
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Efe 4:29
Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu. Badala yake, maneno lazima yatoke katika vinywa vyenu yafaayo kwa mahitaji, kuwapa faida wale wanaosikiliza.Mit 18:21
Uzima na kifo hutawaliwa kwa ulimi, na wale wenye kuupenda ulimi watakula tunda lake.Yak 1:26
Ikiwa mtu yeyote atafikiri mwenyewe kuwa ni mtu wa dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, huudanganya moyo wake na dini yake ni bure.Mit 15:1
Jawabu la upole huondoa ghadhabu, bali neno la ukatili huchochea hasira.Mit 21:23
Anayelinda kinywa chake na ulimi wake hujilinda mwenyewe na taabu.Mit 12:18
Maneno yake asemaye kwa pupa ni kama kurusha upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.Mit 15:4
Ulimi unaoponya ni mti wa uzima, bali ulimi wa udanganyifu huvunja moyo.1 Pet 3:10
“Yeye atakaye kupenda maisha na kuona siku njema lazima auzuie ulimi wake kwa mabaya na midomo yake kusema hila.Zab 141:3
Ee Yahwe, uweke mlinzi kinywani mwangu; mngojezi malangoni pa midomo yangu.Mit 10:19
Katika maneno mengi, hapakosi uhalifu, bali aliyemwangalifu katika usemi wake ni mwenye busara.Yak 3:8
lakini hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye anaweza kudhibiti ulimi; ni uovu usiotulia, umejaa sumu ya kufisha.Zab 19:14
Maneno ya midomo yangu na mawazo ya moyo wangu nayakubalike machoni pako, ewe Yahwe, mwamba wangu na mkombozi wangu.Zab 34:13
Hivyo uepushe ulimi wako na uovu na uilinde midomo yako kuongea uongo.Mt 15:11
Hakuna kitu kiingiacho mdomoni mwa mtu na kumfanya najisi. Bali, kile kitokacho kinywani, hiki ndicho kimfanyacho mtu kuwa najisi.''Mit 16:24
Maneno yenye kufaa ni sega la asali -matamu kwenye nafsi na huponya mifupa.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0