Mwanzo › Biblia inasema nini › Kuwatunza wazazi wazee
Mahusiano
Biblia inasema nini kuhusu Kuwatunza wazazi wazee
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
1 Tim 5:8
Ila kama mtu asipowatunza ndugu zake, hususani wale walioko nyumbani mwake, ameikana imani na ni mmbaya kuliko mtu asiye amini.1 Tim 5:4
Lakini kama mjane ana watoto au wajukuu, waache kwanza wajifunze kuonesha heshima kwa watu wa nyumbani mwao wenyewe. Waache wawalipe wazazi wao mema, kwa kuwa hii inapendeza mbele za Mungu.Kut 20:12
Waheshimu baba na mama yako, ili uweze kuishi miaka mingi duniani Yahweh Mungu wako ametoa.Mit 23:22
Msikilize baba yako ambaye alikuzaa na usimdharau mama yako wakati akiwa mzee.Law 19:32
Ni lazima usimame mbele za mtu mwenye mvi na uheshimu uwepo wa mzee. Yakupasa umwegope Mungu wako. Mimi ndimi Yahweh.Kum 5:16
Mheshimu baba yako na mama yako, kama Yahwe Mungu wako alivyokuamuru kufanya, ili kwamba uweze kuishi muda mrefu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako akupa, ili kwamba iende kwa uzuri kwako.1 Tim 5:1
Usimkemee mwanamume mzee. Bali mtiye moyo kama baba yako. Uwatiye moyo vijana wa kiume kana kwamba ni ndugu zako.Efe 6:2
“Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi),Yn 19:25–27
Askari walifanya mambo haya. Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu. Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!” Kisha akamwambia yule mwanfunzi, “Tazama, huyu hapa mama yako. “Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake.Isa 46:3–4
Nisikilizeni mimi, nyumba ya Yakobo, wote mliobaki kwenye nyumba ya Israeli mliochukuliwa na mimi kutoka kabla amjazaliwa, mlichukuliwa mkiwa tumboni. Hata kwa njie wazee Mimi ndiye, mpaka mmeshapata mvi nitawachukua. Nimewaumba ninyi na nitawabeba ninyi; Nitwachukua nyie na nitawakomboa nyie.Zab 71:9
Usinitupe katika siku za miaka ya uzee wangu; usiniache wakati nguvu zangu zitakapoisha.Yak 1:27
Dini iliyo safi na isiyoharibiwa mbele za Mungu wetu na Baba ni hii: kuwasaidia yatima na wajane katika mateso yao, na kujilinda wenyewe na ufisadi wa dunia.Mt 15:4–6
Kwa kuwa Mungu alisema, 'Mheshimu baba yako na mama yako; na 'Asemaye uovu kwa baba yake na mama yake, hakika atakufa.' Lakini ninyi husema, 'Kila amwambiaye baba yake na mama yake, '“Kila msaada ambao angepata kutoka kwangu sasa ni zawadi kutoka kwa Mungu,''' “Mtu huyo hana haja ya kumuheshimu baba yake. Katika namna hii mmelitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.Mit 23:25
Mfurahishe baba yako na mama yako na yule aliyekuzaa afurahie.Ayu 12:12
Kwa wazee mna hekima; katika wingi wa siku mna ufahamu.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0