Mwanzo › Biblia inasema nini › Ugomvi na kupatana
Mahusiano
Biblia inasema nini kuhusu Ugomvi na kupatana
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Mt 5:9
Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.Mit 15:1
Jawabu la upole huondoa ghadhabu, bali neno la ukatili huchochea hasira.Zab 34:14
Uache uovu na utende mema. Uitafute amani na kuiendea amani.Yak 4:1–2
Ugonvi na migogoro miongoni mwenu vyatoka wapi? Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita ndani ya washirika wenu? Mnatamani kile msichokuwa nacho. Mnauwa na mnafukuzia kile msichoweza kuwa nacho. Mnapigana na kugombana, na bado hampati kwa sababu hamumwombi Mungu.Mt 18:15–17
Kama ndugu yako akikukosea, nenda, kamwonyeshe dosari iliyopo kati yako na yeye akiwa pekee yake. Kama akikusikiliza, utakuwa umemrejesha ndugu yako. Lakini kama hatakusikiliza, mchukue ndugu mmoja au wawili zaidi pamoja nawe, kwa kuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno linaweza kuthibitishwa. Na kama akipuuza kuwasikiliza, liambie kanisa jambo hilo, kama akipuuza vilevile kulisikiliza kanisa, basi na awe kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.Efe 4:26
Mwe na hasira, lakini msitende dhambi.” Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu.Rum 14:19
Kwa hiyo basi, na tufuate mambo ya amani na mambo ambayo humjenga mtu na mwingine.2 Tim 2:23–24
Lakini ukatae upumbavu na maswali ya kipuuzi. Kwani unajua ya kuwa huzaa ugomvi. Mtumishi wa Bwana hapaswi kugombana, badala yake inampasa kuwa mpole kwa watu wote, awezaye kufundisha, na mvumilivu.Rum 12:18
Kama inawezekana, kama ilivyowekwa kwenu, muwe na amani na watu wote.Yak 1:19
Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika,Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0