Mwanzo › Biblia inasema nini › Kuwatia wengine moyo
Mahusiano
Biblia inasema nini kuhusu Kuwatia wengine moyo
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
1 The 5:11
Kwa hiyo, farijianeni na kujengana ninyi kwa ninyi, kama ambavyo tayari mnafanya.Ebr 10:24–25
Na tuzidi kutafakari namna ya kumtia moyo kila mmoja kupenda na matendo mema. Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia.Efe 4:29
Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu. Badala yake, maneno lazima yatoke katika vinywa vyenu yafaayo kwa mahitaji, kuwapa faida wale wanaosikiliza.Mit 12:25
Mashaka katika moyo wa mtu humwelemea, bali neno zuri humfurahisha.Ebr 3:13
Badala yake, mhamasishane kila siku kila mmoja na mwenzie, ili kila iitwapo leo mtamani, ili kwamba mmoja kati yenu asifanywe kuwa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.Gal 6:2
Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.1 The 5:14
Twawasihi, ndugu: muwaonye wasio kwenda kwa utaratibu, watieni moyo walio kata tamaa, Wasaidieni walio wanyonge, na muwe wavumilivu kwa wote.Kol 3:16
Na Neno la Kristo likae ndani yenu kwa utajiri. Kwa hekima yote, fundishaneni na kushauriana ninyi kwa ninyi kwa Zaburi, nyimbo, na nyimbo za rohoni. Imbeni kwa shukrani mioyo yenu kwa Mungu.Mit 27:17
Chuma hunoa chuma; kwa njia ile ile; mtu humnoa rafiki yake.1 The 4:18
Kwa hiyo, mfarijiane ninyi kwa ninyi kwa maneno haya.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0