Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Watoto

Mahusiano

Biblia inasema nini kuhusu Watoto

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (14), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Zab 127:3–5Tazama, wana ni urithi kutoka kwa Yahwe, uzao wa tumbo ni thawabu kutoka kwake. Kama mishale mkononi mwa shujaa, ndivyo walivyo wana wa ujanani. Ni namna gani alivyo barikiwa mtu ambaye amelijaza podo lake hivyo. Hata aibishwa pindi atakapo kabiliana na adui zake katika lango.
Mit 22:6Mfundishe mtoto njia inayompasa na wakati akiwa mzee hatayaacha mafundisho hayo.
Mit 17:6Wajukuu ni taji ya wazee na wazazi huleta heshima kwa watoto wao.
Mt 19:14Bali Yesu akasema, “Waruhusuni watoto wadogo, wala msiwakataze kuja kwangu, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa watu kama wao.
Efe 6:4Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana.
Mt 18:10Tazameni kwamba msije mkamdharau mmoja wa wadogo hawa. Kwa maana nawambieni kuwa mbinguni kuna malaika wao siku zote wakiutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.
Isa 54:13Na watoto wako wote watafundishwa na Yahwe; na amani ya watoto wako itakuwakubwa.
3 Yoh 1:4Sina furaha kubwa zaidi ya hii, kusikia kwamba watoto wangu wanatembea katika kweli.
Yn 16:21Mwanamke anakuwa na huzuni wakati anapokuwa na uchungu kwa sababu wakati wa kujifungua umefika; lakini anapojifungua mtoto, hakumbuki tena maumivu kwa sababu ya furaha yake kwamba mtoto amezaliwa duniani.
Mt 18:1–3Muda huo huo wanafunzi wakaja kwa Yesu na kumwambia, “Ni nani aliye mkubwa katika ufalme wa mbinguni?” Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao, na kusema, “Kweli nawaambieni, msipotubu na kuwa kama watoto wadogo hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.
Mwa 1:28Mungu akawabariki na akawaambia, “zaeni na kuongezeka. Jazeni nchi, na muitawale. Muwe na mamlaka juu ya samaki wa baharini, juu ya ndege wa angani, na juu ya kila kiumbe hai kiendacho juu ya nchi,”
Zab 113:9Humpa watoto wanamke aliye tasa, humfanya yeye kuwa mama wa watoto mwenye furaha. Msifuni Yahwe!
Kol 3:21Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa.
Mit 13:24Yeye ambaye hamrudi mwanawe humchukia, bali yule anayempenda mwanawe humjali kwa kumwadibisha.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0