Mwanzo › Biblia inasema nini › Kuwaheshimu wazazi wako
Mahusiano
Biblia inasema nini kuhusu Kuwaheshimu wazazi wako
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Kut 20:12
Waheshimu baba na mama yako, ili uweze kuishi miaka mingi duniani Yahweh Mungu wako ametoa.Efe 6:1
Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki.Efe 6:2–3
“Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi), “ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu juu ya nchi.”Kum 5:16
Mheshimu baba yako na mama yako, kama Yahwe Mungu wako alivyokuamuru kufanya, ili kwamba uweze kuishi muda mrefu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako akupa, ili kwamba iende kwa uzuri kwako.Kol 3:20
Watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, maana ndivyo impendezavyo Bwana.Mit 23:22
Msikilize baba yako ambaye alikuzaa na usimdharau mama yako wakati akiwa mzee.Law 19:3
Kila mtu amstahi mama yake na baba yake. Na ni lazima muzishike Sabato zangu. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.Mk 7:10
Kwa kuwa Musa alisema, 'mheshimu baba yako na mama yako,' na 'Yeye asemaye mabaya juu ya baba yake au mama yake hakika atakufa.'Mit 1:8
Mwanangu, sikia fundisho la baba yako na wala usiziache kanuni za mama yako;Mt 19:19
waheshimu baba yako na mama yako, na mpende jirani yako kama nafsi yako.”Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0