Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Umbea

Mahusiano

Biblia inasema nini kuhusu Umbea

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (12), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Mit 16:28Mtu mkaidi huchochea mafarakano na umbeya huwafarakanisha marafiki.
Mit 26:20Kwa kukosa kuni, moto huzimika; na pale pasipo na mmbea ugomvi hukoma.
Mit 20:19Mmbea hufunua siri na kwa hiyo hupaswi kushirikiana na watu ambao huongea sana.
1 Tim 5:13Na pia huingia kwenye mazoea ya uvivu. Wao huzunguka nyumba kwa nyumba. Si tu kwamba ni wavivu, bali pia huwa wasengenyaji na na wenye kuingilia mambo ya wengine. Wao husema mambo wasiyopaswa kuyasema.
Mit 11:13Anayekwenda akizunguka kwa kukashifu hufunua siri, bali mtu mwaminifu hustiri jambo.
Law 19:16Usiende huku na huko ukisema habari za uchochezi miongoni mwa watu wako, bali tafuta kuyalinda maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Yahweh.
Mit 18:8Maneno ya mmbea ni kama chembe tamu na hushuka katika sehema za ndani sana kwenye mwili.
Mit 10:18Yeye afichaye chuki anamidomo ya uongo, na yeye anayesambaza kashfa ni mpumbavu.
Kut 23:1Haupaswi kutoa taarifa ya uongo kuhusu yeyote. usijiunge na mwanaume muovu kuwa shahidi wa uongo.
Yak 4:11Msineneane kinyume ninyi kwa ninyi, ndugu. Mtu anenaye kinyume na ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, hunena kinyume na sheria na huihukumu sheria ya Mungu. Mkiihukumu sheria, hamuitii sheria, bali mnaihukumu.
Zab 101:5Nitamwangamiza yeyote amsengenyaye jirani yake kwa siri. Sitamvumilia yeyote mwenye kiburi.
Mt 12:36Nawaambia kuwa katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu ya kila neno lisilo na maana walilosema.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0