Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Wema

Mahusiano

Biblia inasema nini kuhusu Wema

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Efe 4:32Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Kol 3:12Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Lk 6:35Lakini wapendeni adui zenu na watendeeni mema. Wakopesheni na msihofu kuhusu kurudishiwa, na thawabu yenu itakuwa kubwa. Mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwasababu yeye mwenyewe ni mwema kwa watu wasio na shukurani na waovu.
Mit 11:17Mtu mkarimu hufaidika mwenyewe, bali mkatili hujiumiza mwenyewe.
Mt 7:12Kwa sababu hiyo, unapotaka kufanyiwa kitu chochote na watu wengine, nawe pia itakupasa kuwafanyia hivyo hivyo wao. Kwa kuwa hiyo ni sheria na manabii.
Mk 6:34Walipofika pwani, aliona umati mkubwa na akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Na akaanza kuwafundisha mambo mengi.
1 Kor 13:4Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi
Gal 6:2Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.
Mit 19:17Mwenye ukarimu kwa masikini humkopesha Yehova na atalipwa kwa kile alichofanya.
1 Yoh 3:18Watoto wangu wapenzi, tusipende kwa midomo wala kwa maneno matupu bali katika vitendo na kweli.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0