Mwanzo › Biblia inasema nini › Usaliti na maumivu
Mahusiano
Biblia inasema nini kuhusu Usaliti na maumivu
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Mik 7:5–6
Msimwamini kila jirani; msimuweke kiongozi katika rafiki yeyote. Kuweni makini kuhusiana na kile msemacho hata kwa mwanamke ambaye adanganyaye kwenye mikono yenu. Kwa kuwa mwana humfedhehesha baba yake, binti huinuka kushindana na mama yake, na mke wa mwana wa kiume hushindana na mama mkwe wake. Adui wa watu ni watu wa nyumba yake mwenyewe.Mk 11:25
Wakati mnaposimama na kuomba, mnapaswa kusamehe chochote mlichonacho dhidi ya yeyote, ili kwamba Baba yenu aliye mbinguni awasamehe pia ninyi makosa yenu.Zab 118:8
Ni bora kuwa na makazi katika Yahwe kuliko kumtumainia mwanadamu.Mt 6:14–15
Ikiwa mtawasemehe watu makosa yao, Baba yako aliye mbinguni pia atawasamehe ninyi. Lakini ikiwa hamtawasamehe makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.Zab 34:18
Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.Lk 6:27
Lakini nasema kwenu ninyi mnaonisikiliza, wapendeni adui zenu na kufanya mema kwa wanao wachukieni.Zab 41:9
Kweli, hata rafiki yangu wa karibu, ambae nilimuamini, aliye kula mkate wangu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.Lk 21:16
Lakini mtakataliwa pia na wazazi wenu, ndugu zenu, jamaa zenu na rafiki zenu, na watawaua baadhi yenu.Lk 22:48
lakini Yesu akamwambia, “Yuda, je unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”Rum 12:19
Wapenzi, msijilipizie kisasi wenyewe, lakini ipisheni ghadhabu ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, '' 'kisasi ni changu; Mimi nitalipa,' asema Bwana.”Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0