Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Kuwakaribisha wageni

Mahusiano

Biblia inasema nini kuhusu Kuwakaribisha wageni

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Ebr 13:2Msisahau kuwakaribisha wageni, maana kwa kufanya hivi, baadhi wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
1 Pet 4:9Onyesheni ukarimu kwa kila mmoja bila kunung'unika.
Rum 12:13Mshiriki katika mahitaji ya waumini. Tafuteni njia nyingi za kuonesha ukarimu.
Law 19:34Mgeni anayeishi pamoja nanyi ni lazima awe kama mwenyeji Mwisraeli mzaliwa anayeishi kwenu, na sharti umpende kama unavyojipenda wewe mwenyewe, ni kwa sababu wewe ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.
Lk 14:12–14Yesu pia alimwambia mtu aliyemwalika, 'Unapotoa chakula cha mchana au cha jioni, usiwaalike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako matajiri, ili kwamba wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Badala yake, unapofanya sherehe, waalike maskini, vilema, viwete na vipofu, na wewe utabarikiwa, kwa sababu hawawezi kukulipa. Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.”
Mdo 28:2Watu wenyeji wa pale si tu kwamba walitupa ukarimu wa kawaida, bali waliwasha moto na kutukaribisha sote, kwa sababu ya mvua na baridi iliyokuwa ikiendelea.
Mk 9:41Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu uko na Kristo, kweli nawaambia, hatapoteza thawabu yake.
Mt 25:35Kwa kuwa nilikuwa na njaa na mlinipa chakula; Nilikuwa mgeni na mlinikaribisha;
Kum 10:19Kwa hiyo basi mpende mgeni; kwa kuwa mlikuwa wageni kutoka nchi ya Misri.
Mt 25:40Na mfalme atawajibu na kuwaambia, 'Kweli nawaambia, mlichotenda hapa kwa mmoja wa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.'

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0