Mwanzo › Biblia inasema nini › Kuwapenda adui zako
Mahusiano
Biblia inasema nini kuhusu Kuwapenda adui zako
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (12), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Lk 6:27–28
Lakini nasema kwenu ninyi mnaonisikiliza, wapendeni adui zenu na kufanya mema kwa wanao wachukieni. Wabarikini wale wanao walaani ninyi na waombeeni wale wanaowaonea.Mt 5:44
Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi,Rum 12:20
“Lakini ikiwa adui yako ana njaa, mlishe. Akiwa na kiu, mnyweshe. Kwa maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto juu ya kichwa chake.”Mit 24:17
Usisherekee wakati adui yako anapoanguka na wala moyo wako usifurahi anapojikwaa,Rum 12:14
Watakieni baraka wote wanaowatesa ninyi; muwabariki na wala msiwalaani.Mt 5:38–39
Mmesikia imenenwa kuwa, 'Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.' Lakini mimi namwambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na jingine pia.Lk 23:34
Yesu alisema, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. “Nao wakapiga kura, kugawa mavazi yake.Mit 16:7
Njia za mtu zinapompendeza Yehova, huwafanya hata adui zake huyo mtu wawe na amani naye.Rum 12:19
Wapenzi, msijilipizie kisasi wenyewe, lakini ipisheni ghadhabu ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, '' 'kisasi ni changu; Mimi nitalipa,' asema Bwana.”Lk 6:35
Lakini wapendeni adui zenu na watendeeni mema. Wakopesheni na msihofu kuhusu kurudishiwa, na thawabu yenu itakuwa kubwa. Mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwasababu yeye mwenyewe ni mwema kwa watu wasio na shukurani na waovu.Mk 11:25
Wakati mnaposimama na kuomba, mnapaswa kusamehe chochote mlichonacho dhidi ya yeyote, ili kwamba Baba yenu aliye mbinguni awasamehe pia ninyi makosa yenu.Mt 6:14–15
Ikiwa mtawasemehe watu makosa yao, Baba yako aliye mbinguni pia atawasamehe ninyi. Lakini ikiwa hamtawasamehe makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0