Gundua › Injili kando kwa kando › Katika Galilaya
Injili kando kwa kando · Katika Galilaya
Mama na ndugu zake Yesu
Mt 12:46–50 · Mk 3:31–35 · Lk 8:19–21
Mt 12:46–5046Wakati Yesu alipokuwa akizungumza na umati tazama, mama yake na ndugu zake walisimama nje, wakitafuta kuongea naye.
47Mtu mmoja akamwambia, “Tazama mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanatafuta kuongea nawe”.
48Lakini Yesu alijibu na kumwambia aliyemjulisha, “Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?”
49Naye alinyoosha mkono wake kwa wanafunzi na kusema, “Tazama, hawa ni mama na ndugu zangu!
50Kwa kuwa yeyote afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, mtu huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu”.
Mk 3:31–3531Kisha mama yake na ndugu zake walikuja na kusimama nje. Wakamtuma mtu, kumwita.
32Na umati wa watu uliokuwa umekaa karibu naye wakamwambia, “mama yako na ndugu zako wako nje, na wanakutafuta wewe”.
33Aliwajibu, “Ni nani mama yangu na ndugu zangu?”
34Aliwaangalia waliokuwa wamekaa wamemzunguka, na akasema, “Tazama, hawa ni mama zangu na ndugu zangu!
35Yeyote afanyaye mapenzi ya Mungu, mtu huyo ni ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu”.
Lk 8:19–2119baadaye mama yake Yesu na ndugu zake wakaja kwake hawakaribia kwa sababu ya umati wa watu.
20Na akataarifiwa, “Mama yako na ndugu zako wako pale nje wanahitaji kukuona wewe.
21Lakini, Yesu akajibu akasema “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY