Gundua › Injili kando kwa kando › Katika Galilaya
Injili kando kwa kando · Katika Galilaya
Ishara ya Yona
Mt 12:38–42 · Lk 11:29–32
Mt 12:38–4238Kisha baadhi ya waandishi na Mafarisayo walimjibu Yesu wakisema” Mwalimu, tungependa kuona ishara kutoka kwako.”
39Lakini Yesu alijibu na kuwaambia, “Kizazi kiovu na cha zinaa kinatafuta ishara. Lakini hakuna ishara itakayotolewa kwao isipokuwa ile ishara ya Yona nabii.
40Kama vile nabii Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu mchana na usiku, hivyo ndivyo Mwana wa Adam atakavyo kuwa ndani ya moyo wa nchi kwa siku tatu mchana na usiku.
41Watu wa Ninawi watasimama mbele ya hukumu pamoja na kizazi cha watu hawa na watakihukumu. Kwa kuwa walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, mtu fulani mkuu kuliko Yona yuko hapa.
42Malkia wa kusini atainuka kwenye hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki na kukihukumu. Alikuja toka miisho ya dunia kuja kusikia hekima ya Selemani, na tazama, mtu fulani mkuu kuliko Selemani yupo hapa.
Lk 11:29–3229Wakati umati wa watu wanakusanyika na kuongezeka, Yesu akaanza kusema “ Kizazi hiki ni kizazi cha uovu. Hutafuta ishara, na hakuna ishara watayopewa zaidi ya ile ishara ya Yona.
30Maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki
31Malkia wa Kusini atasimama siku ya hukumu na watu wa kizazi hiki na kuwahukumu wao, kwani yeye alitoka katika mwisho wa nchi ili aje asikilize hekima za Solomoni, na hapa yuko aliye mkuu kuliko Solomoni.
32Watu wa Ninawi watasimama katika hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki siku ya hukumu watakihukumu, kwani wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, hapa yuko aliye mkuu kuliko Yona.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY