Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mwanzo

Injili kando kwa kando · Mwanzo

Yesu aanza kuhubiri Galilaya

Mt 4:12–17 · Mk 1:14–15 · Lk 4:14–15

Mathayo

Mt 4:12–17

12Basi Yesu aliposikia kuwa Yohana amekamatwa, aliondoka mpaka Galilaya.

13Aliondoka Nazareti alienda na kuishi Kaperanaumu, iliyoko kandokando na Bahari ya Galilaya, mipakani mwa majimbo ya Zabuloni na Naftali.

14Hii ilitokea kutimiza kile kilichonenwa na nabii Isaya,

15“Katika mji wa Zabuloni na mji wa Naftali, kuelekea Baharini, ng'ambo ya Yorodani, Galilaya ya wamataifa!

16Watu walio kaa gizani wameuona mwanga mkuu, na wale waliokuwa wameketi katika maeneo na kivuli cha mauti, juu yao nuru imewaangazia.''

17Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri na kusema, “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''

Marko

Mk 1:14–15

14Sasa baada ya Yohana kukamatwa, Yesu alikuja Galilaya akitangaza injili ya Mungu,

15akisema, “Muda umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuamini katika injili”.

Luka

Lk 4:14–15

14Kisha Yesu alirudi Galilaya kwa nguvu za Roho, na habari kumhusu yeye zikaenea na kusambaa katika mikoa jirani yote.

15Alifundisha katika masinagogi yao, na kila mmoja alimsifu.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY