Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mateso

Injili kando kwa kando · Mateso

Mmoja wenu atanisaliti

Mt 26:20–25 · Mk 14:17–21 · Lk 22:21–23 · Yn 13:21–30

Mathayo

Mt 26:20–25

20Ilipofika jioni, aliketi kula chakula pamoja na wale wanafunzi Kumi na Wawili.

21Walipokuwa wanakula chakula, alisema, “Kweli nawaambia kwamba mmoja wenu atanisaliti.”

22Walihuzunika sana, na kila mmoja alianza kumuuliza, “Je, hakika siyo mimi, Bwana?”

23Akawajibu, “Yule ambaye anachovya mkono wake pamoja nami katika bakuli ndiye atakaye nisaliti.

24Mwana wa Adamu ataondoka, kama alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu ambaye atamsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa vizuri kwa mtu huyo kama asingezaliwa.”

25Yuda, ambaye angemsaliti alisema, “Je!, Ni mimi Rabi?” Yesu akamwambia, “Umesema jambo hilo wewe mwenyewe.”

Marko

Mk 14:17–21

17Wakati ilipokuwa jioni, alikuja na wale Kumi na wawili.

18Na walipokuwa wakiikaribia meza na kula, Yesu alisema, “Kweli nawaambia, mmoja kati yenu anayekula pamoja nami atanisaliti.”

19Wote walisikitika, na mmoja baada ya mwingine walimwambia, “Hakika siyo mimi?”

20Yesu alijibu na kuwaambia, “Ni mmoja wa Kumi na wawili kati yenu, mmoja ambaye sasa anachovya tonge katika bakuli pamoja nami.

21Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakwenda kama vile maandiko yasemavyo juu yake. Lakini ole wake mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu atasalitiwa! Ingekuwa vizuri zaidi kwake kama mtu yule asingezaliwa.”

Luka

Lk 22:21–23

21Lakini angalieni. Yule anisalitie yuko pamoja nami mezani.

22Kwa maana Mwana wa Adamu kwa kweli aenda zake kama ilivyokwisha amuliwa. Lakini ole kwa mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu asalitiwa!”

23Wakaanza kuulizana wao kwa wao, nani miongoni mwao ambaye angefanya jambo hili.

Yohana

Yn 13:21–30

21Wakati Yesu aliposema haya, alisumbuka rohoni, alishuhudia na kusema, “Amini, amini, nawambia kwamba mmoja wenu atanisaliti.”

22Wanafunzi wake wakatazamana, wakishangaa ni kwa ajili ya nani alizungumza.

23Kulikuwa katika meza, mmoja wa wanafunzi wake ameegama kifuani mwa Yesu yule ambaye Yesu alimpenda.

24Simoni Petro alimuuliza mwanafunzi huyu na kusema, “Twambie ni yupi ambaye kwake anazungumza.”

25Mwanafunzi yule aliye egama kifuani mwa Yesu na akamwambia, “Bwana, ni nani?”

26Kisha Yesu alijibu, “Ni kwake yule nitakaye chovya kipande cha mkate na kumpatia.” Hivyo alipo kuwa amechovya mkate, alimpatia Yuda mwana wa Simon Iskariote.

27Na baada ya mkate, Shetani alimuingia. Kisha Yesu akamwambia, “Kile ambacho unataka kukifanya ukifanye haraka.”

28Sasa hakuna mtu katika meza alijua sababu ya Yesu kusema jambo hili kwake.

29Baadhi yao walidhani kwamba, kwa sababu Yuda alishika mfuko wa fedha, Yesu alimwambia, “Nunua vitu tunavyohitaji kwa ajili ya sikukuu,” au kwamba anapaswa kutoa kitu kwa masikini.

30Baada ya Yuda kupokea mkate, alitoka nje harak; na ilikuwa usiku.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY