Klaudio aliitawala milki na kuiongezea Uingereza baada ya uvamizi wa mwaka 43 B.K. Matendo 18:2 inasema kwamba aliamuru Wayahudi wote waondoke Roma; mwandishi Mrumi Suetonio pia anataja kufukuzwa huko.
Ensaiklopidia › Wakati huo duniani
Katika Biblia · karibu 50 B.K. · Athene
Paulo huko Athene
Kati ya mahekalu na wanafalsafa wa Athene, Paulo anahutubu katika Areopago kuhusu “mungu asiyejulikana.”
Na wakati akiwasubiri huko Athene, roho yake ilikasirishwa ndani yake kwa jinsi alivyouona mji ulivyojaa sanamu nyingi. Hivyo akajadiliana katika sinagogi na wayahudi wale waliomcha Mungu na kwa wale wote aliokutana nao kila siku sokoni. Lakini baathi ya Wanafalsafa wa Waepikureo na Wastoiko wakamkabili. Na wengine wakasema, “ Ni nini anachokisema huyu mwongeaji mchanga? Wengine wakasema, “inaonekana anahubiri habari ya mungu mgeni,” kwasababu anahubiri habari ya Yesu na ufufuo. Wakamchukua Paulo na kumleta Areopago, wakisema, “Twaweza kujua haya mafundisho mapya unayoyaongea? Kwasababu unaleta mambo mapya katika masikio yetu. Kwahivyo tunataka kujua haya mambo yana maana gani?” (Na watu wote wa Athene pamoja na wageni waliopo kwao, hutumia muda wao aidha katika kuongea na kusikiliza juu ya jambo jipya.) Kwa hiyo Paulo akasimama katikati ya watu wa Areopago na kusema, “Enyi watu wa Athene, naona kuwa ninyi ni watu wa dini kwa kila namna, Kwani katika kupita kwangu na kuangalia vitu vyenu vya kuabudu, nimeona maneno yalioandikwa kwenye moja ya madhabahu yenu, ikisema “KWA MUNGU ASIYEJULIKANA”. Hivyo basi, huyo mnayemwabudu pasipokujua, ndiye ninayewajulisha ninyi. Mungu aliyeumba dunia na kila kitu kilichoko ndani, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hawezi kukaa katika mahekalu yaliyotengenezwa na mikono. Na pia hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu kwao, kwani yeye mwenyewe huwapa watu uzima na pumzi na vitu vingine vyote. Kupitia mtu mmoja, alifanya mataifa yote ya watu waishio juu ya uso wa dunia, na akawawekea nyakati na mipaka katika maeneo wanaoishi. Kwa hiyo, wanatakiwa kumtafuta Mungu, na yamkini wamfikie na kumpata, na kwa uhakika hayupo mbali na kila mmoja wetu. Kwake tunaishi, tunatembea na kuwa na uzima wetu, kama vile mtunzi wenu mmoja wa shairi aliposema 'tu wazaliwa wake.' Kwa hiyo, ikiwa sisi ni wazaliwa wa Mungu, hatupaswi kufikiri kuwa uungu ni kama dhahabu, au shaba, au mawe, sanamu iliyochongwa kwa ustadi na mawazo ya watu. Kwa hiyo, Mungu alinyamazia nyakati zile za ujinga, lakini sasa anaamuru watu wote kila mahali wapate kutubu. Hii ni kwa sababu ameweka siku atakayo ihukumu dunia kwa haki kwa mtu ambaye alimchagua. Mungu alitoa uhakika wa mtu huyu kwa kila mtu pale alipomfufua katoka kwa wafu. Na watu wa Athene waliposikia habari ya kufufuliwa kwa wafu, baadhi yao wakamdhihaki Paulo, ila wengine wakasema “Tutakusikiliza tena kwa habari ya jambo hili” Baada ya hapo, Paulo akawaacha. Lakini baadhi ya watu waliungana naye wakaamini, akiwemo Dionisio Mwareopago, na Mwanamke anaitwa Damari na wengine pamoja nao.Wakati huo duniani
Paulo alifika Athene karibu 50 B.K., katika safari iliyompeleka hadi Korintho, ambako maandishi yaliyopatikana Delfi yanaweka tarehe ya liwali Galio karibu 51–52 B.K. (Matendo 18:12). Athene wakati huo ulikuwa mji wa kawaida wa Milki ya Roma, ingawa bado maarufu kwa wanafalsafa wake. Huu ndio ulimwengu wa karibu 50 B.K.
Mwanafalsafa Mstoiki Seneka, mwalimu wa Nero kijana, aliandika insha kuhusu hasira, ufupi wa maisha na utulivu wa moyo. Kaka yake mkubwa alikuwa Galio, liwali ambaye Paulo aliletwa mbele yake huko Korintho (Matendo 18:12).
Kaisari Guangwu alirudisha nasaba ya Han na kuhamishia mji mkuu wake Luoyang. Katika mwaka wake wa mwisho, 57 B.K., wajumbe walikuja kutoka Wa, huko Japani; muhuri wa dhahabu uliopatikana Japani mwaka 1784 unadhaniwa kuwa ndio aliowapa.
Kwa mapokeo ya Wakristo wa Mtakatifu Tomaso wa Kerala, mtume Tomaso alitua karibu na Muziris mwaka 52 B.K. Masimulizi ya zamani zaidi, Matendo ya Tomaso, yanamweka katika baraza la Gondophares, mfalme wa kaskazini-magharibi mwa India ambaye sarafu zake zimepatikana.
Huko Aleksandria mwanafalsafa Myahudi Filo alieleza vitabu vya Musa kwa lugha ya falsafa ya Kigiriki. Mwaka 40 B.K. aliongoza ujumbe wa Wayahudi wa mji huo kwa Kaisari Kaligula baada ya ghasia dhidi yao.
Huko Meroe, kando ya Nile katika Sudan ya leo, ufalme wa Kushi mara nyingi ulitawaliwa na malkia waliobeba cheo cha kandake — “kandase” wa Matendo 8:27. Watawala wake walizikwa chini ya piramidi ndogo zenye mteremko mkali.
Kwenye uwanda wa jangwa wa kusini mwa Peru, watu wa Nazca walichora mistari na maumbo makubwa sana — ndege mvumaji, tumbili, buibui — kwa kuondoa mawe meusi ya juu. Mengi yanaonekana vizuri zaidi kutoka angani au kutoka vilima vya karibu.