Moto uliwaka kwa siku kadhaa na kuteketeza sehemu kubwa ya mji. Mwanahistoria Tacitus anaandika kwamba Nero aliwasingizia Wakristo na kuamuru wengi wao wauawe — mateso ya kwanza yanayojulikana ya Wakristo yaliyofanywa na Roma.
Ensaiklopidia › Wakati huo duniani
Katika Biblia · karibu 60–62 B.K. · Rumi
Paulo huko Rumi
Baada ya kuvunjikiwa merikebu huko Malta Paulo anafika Rumi, anakoishi kwa miaka miwili chini ya ulinzi, akiwapokea wageni.
Baada ya miezi mitatu, tulisafiri ndani ya meli ya Iskanda ambayo ilikuwa imepigwa baridi hapo kisiwani, ambayo viongozi wake walikuwa ndugu wawili mapacha. Baada ya kuwa tumetua katika mji wa Sirakusa, tulikaa pale siku tatu. Kutokea pale tulisafiri tukafika katika mji wa Regio. Baada ya siku moja upepo wa kusini ulitokea ghafla, na baada ya siku mbili tukafika katika mji wa Putoli. Huko tuliwakuta baadhi ya ndugu na tulikaribishwa kukaa nao kwa siku saba. Kwa njia hii tukaja Rumi. Kutoka huko wale ndugu, baada ya kuwa wamesikia habari zetu, walikuja kutupokea huko soko la Apias na Hotel tatu. Paulo alipowaona wale ndugu alimshukuru Mungu akajitia ujasiri. Tulipoingia Roma, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake pamoja na yule askari aliyekuwa akimlinda. Basi ilikuwa baada ya siku tatu Paulo aliwaita pamoja wale wanume waliokuwa viongozi kati ya Wayahudi. Walipokuja pamoja, alisema kwao, “Ndugu, pamoja na kwamba sijafanya kosa lolote kwa watu hawa au kufanya kinyume na taratibu za mababa zetu waliotutangulia, nilitolewa kama mfungwa kutoka Yerusalemu hadi kwenye mikono ya Warumi. Baada ya kunihoji, walitamani kuniacha huru, kwa sababu kulikuwa hakuna sababu kwangu mimi ya kustahili adhabu ya kifo. Lakini wale Wayahudi walipoongea kinyume cha shauku yao, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisaria, japokuwa haikuwa kana kwamba naleta mashtaka juu ya taifa langu. Kwa sababu ya kukata kwangu rufaa, hivyo, niliomba kuwaona na kuongea nanyi. Ni kwa sababu ya kile ambacho Israel anaujasiri kwacho, nimefungwa na kifungo hiki. Kisha wakamwambia, “Hatujawahi kupokea barua kutoka Yudea kukuhusu wewe, wala hakuna ndugu aliyekuja na kutoa taarifa au kusema neno lolote baya kuhusu wewe. Lakini tunataka kusikia kutoka kwako unafikiri nini kuhusu hili kundi la watu hawa, kwa sababu inajulikana kwetu kwamba linaongea kinyume kila mahali.” Walipokuwa wametenga siku kwa ajili yake, watu wengi zaidi walimwijia mahali alipokuwa anaishi. Alisema lile jambo kwao na kushuhudia kuhusu ufalme wa Mungu. Alijaribu kuwashawishi kuhusu Yesu, kwa namna zote mbili kutoka katika sheria za Musa na kutoka kwa manabii, kuanzia asubuhi hadi jioni. Baadhi yao walishawishika kuhusu mambo yale yaliyosemwa, wakati wengine hawakuamini. Waliposhindwa kukubaliana wao kwa wao, waliondoka baada ya Paulo kulisema jambo hili moja, “Roho Mtakatifu alisema vyema kupitia Isaya nabii kwa baba zenu. Alisema, 'Nenda kwa watu hawa useme, “Kwa masikio yenu mtasikia, lakini hamtaelewa; Na kwa macho yenu mtaona lakini hamtatambua. Kwa ajili ya mioyo ya watu hawa imekuwa dhaifu, masikio yao yamesikia kwa taabu, wamefumba macho yao; ili kwamba wasijekutambua kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kuelewa kwa mioyo yao, na kugeuka tena, na ningeliwaponya.”' Kwa hiyo, mnapaswa kujua kwamba huu wokovu wa Mungu umepelekwa kwa watu wa Mataifa, na watasikiliza.” (Zingatia: Mstari huu “Wakati alipokuwa amesema mambo haya, wayahudi waliondoka, wakiwa na mashindano makubwa kati yao.,” haumo kwenye nakala bora za kale). Paulo alikaa katika nyumba yake ya kupanga kwa miaka yote miwili, na aliwakaribisha wote waliokuja kwake. Alikuwa akihubiri ufalme wa Mungu na alikuwa akifundisha mambo juu ya Bwana Yesu Kristo kwa ujasiri wote. Hakuna aliyemzuia.Wakati huo duniani
Kitabu cha Matendo kinaishia na Paulo akiwa chini ya ulinzi huko Roma kwa miaka miwili, karibu 60–62 B.K., akifundisha waziwazi katika nyumba aliyoipanga (Matendo 28:30–31). Maliki alikuwa Nero. Huu ndio ulimwengu wa miaka ya 60 B.K.
Huko Britania, Malkia Boudica wa kabila la Iceni aliongoza uasi mkubwa na kuuchoma moto Londinium — mji mchanga wa Kirumi ambao ulikuja kuwa London — kabla Warumi hawajamshinda.
Huko Aleksandria mhandisi Heroni alieleza mpira unaozungushwa na mvuke na mashine zinazoendeshwa na hewa na maji. Kwa kawaida wakati wake hukadiriwa kwa kupatwa kwa mwezi anakokutaja, ambako kunalingana na kule kwa mwaka 62 B.K.
Kwa mapokeo ya China, maliki Ming wa Han aliota ndoto ya umbo la dhahabu na kutuma wajumbe magharibi. Walirudi na watawa wa Kibuddha na maandiko, na Hekalu la Farasi Mweupe likajengwa kwa ajili yao huko Luoyang — hekalu la kwanza la Kibuddha nchini China.
Wafalme wa Kushani kutoka Asia ya Kati walijenga milki iliyoenea katika Afghanistan, Pakistan na kaskazini mwa India ya leo. Nchi zao zilikuwa kwenye njia zilizounganisha Roma, India na China.
Kumbukumbu za Kale za Kyiv, zilizokusanywa karibu mwaka 1110, zinasimulia kwamba mtume Andrea alisafiri kwa chombo kupanda mto Dnieper, akasimika msalaba juu ya vilima ambapo Kyiv ingesimama, na akatabiri kwamba mji mkubwa ungekuwa pale. Wanahistoria wanaliona hili kuwa hekaya; mapokeo ya zamani zaidi yanampa Andrea Skithia kama eneo la utume wake.