Mwanzo › Biblia inasema nini › Shukrani
Hisia
Biblia inasema nini kuhusu Shukrani
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
1 The 5:18
Mshukuruni Mungu kwa kila jambo, kwa sababu hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Yesu Kristo.Efe 5:20
Daima toa shukrani kwa mambo yote katika jina la Kristo Yesu Bwana wetu kwa Mungu Baba.Kol 3:15
Amani ya Kristo na iwaongoze mioyoni mwenu. Ilikuwa ni kwa ajili ya amani hii kwamba mliitiwa katika mwili mmoja. Iweni na shukrani.Zab 107:1
Mshukuruni Yahwe, maana ni mwema, na uaminifu wa agano lake wadumu milele.Zab 106:1
Msifuni Yahwe. Mshukuruni Yahwe, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.Yak 1:17
Kila zawadi iliyo nzuri na kila zawadi iliyokamilika hutoka juu, hushuka chini kutoka kwa Baba wa nuru. Kamwe habadiliki kama kivuli kibadilikavyo.Zab 100:4
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni yeye na litukuzeni jina lake.Flp 4:6
Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali, kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu.Kol 3:17
Na chochote mfanyacho, katika maneno au katika matendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu. Mpeni shukrani Mungu baba kupitia Yeye.Kol 4:2
Endeleeni kuwa thabiti katika maombi. Kaeni macho katika hilo kwa shukrani.Zab 118:24
Hii ni siku ambayo Yahwe ametenda; tutaifurahia na kuishangilia.Zab 136:1
Oh, mshukuruni Yahwe; kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.1 Nya 16:34
Toeni shukurani kwa Yahweh, kwa kuwa ni mwema, uaminifu wa agano lake la dumu ata milele.Zab 69:30
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo na nitamtukuza yeye kwa shukrani.Zab 28:7
Yahwe ni nguvu yangu na ngao yangu; moyo wangu wa humwamini yeye, na ninasaidiwa. Kwa hiyo moyo wangu hufurahia sana, nami nitamsifu yeye kwa kuimba.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0