Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Zaburi 150

Mstari wa Biblia · ULB

Zaburi 150

1Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu za ukuu wake.

2Msifuni yeye kwa matendo yake makuu; msifuni yeye kwa kadri ya wingi wa ukuu wake.

3Msifuni kwa mlipuko wa pembe; msifuni kwa kinanda na kinubi.

4Msifuni kwa ngoma na kucheza; msifuni kwa vyombo vya nyuzi na filimbi.

5Msifuni kwa matoazi yavumayo; msifuni kwa matoazi avumayo sana.

6Kila kilicho na pumzi kimsifu Yahwe. Msifuni Yahwe.

Soma sura nzima: Zaburi 150

Kwa Kiingereza

Berean Standard BiblePsalm 150Hallelujah! Praise God in His sanctuary. Praise Him in His mighty heavens. Praise Him for His mighty acts; praise Him for His excellent greatness. Praise Him with the sound of the horn; praise Him with the harp and lyre. Praise Him with tambourine and dancing; praise Him with strings and flute. Praise Him with clashing cymbals; praise Him with resounding cymbals. Let everything that has breath praise the LORD! Hallelujah!

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Zab 145:21Kinywa changu kitazinena sifa za Yahwe; wanadamu wote na walitukuze jina lake takatifu milele na milele.
Ufu 5:13Nikasikia kila kilichoumbwa kilichokuwa mbinguni na duniani na chini ya nchi na juu ya bahari, kila kitu ndani yake kikisema, “Kwake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi na kwa mwanakondoo, kuwe sifa, heshima, utukufu na nguvu ya kutawala milele na milele.”
Zab 103:22Msifuni Yahwe, viumbe wake wote, mahali popote atawalapo. Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote.
Zab 145:10Vyote ulivyo viumba vitakushukuru wewe, Yahwe; waaminifu wako watakutukuza wewe.
Zab 148:7–11Msifuni yeye kutoka nchi, ninyi viumbe wa baharini na viumbe vyote katika kina cha bahari, moto na mvua ya mawe, theluji na mawingu, upepo wa dhoruba ukitimiza neno lake. Msifuni yeye, enyi milima na vilima, miti ya matunda na mierezi yote, wanyama pori na wanyama wafugwao, viumbe vitambaavyo na ndege. Msifuni Yahwe, wafalme wa nchi na mataifa yote, wakuu na watawala wote wa nchi,
Zab 149:1Msifuni Yahwe. Mwimbieni Yahwe wimbo mpya; imbeni sifa zake katika kusanyiko la waaminifu.
Zab 134:2Inueni mikono yenu patakatifu pake na mtukuzeni Yahwe.
Kum 3:24'O Bwana Yahwe, umeanza kumuonesha mtumwa wako ukuu wako na mkono wako wa hodari; kwa kuwa nani mungu aliyeko huko mbinguni au duniani ambaye anaweza kufanya kazi zilezile kama ilivyofanya, na matendo yaleyale makuu?

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki