Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Zaburi 1

Mstari wa Biblia · ULB

Zaburi 1

1Amebarikiwa mtu yule asiye enenda katika ushauri wa waovu, au kusimama katika njia ya wenye dhambi, au kukaa katika kusanyiko la wenye mizaha.

2Bali yeye huifurahia sheria ya Yahwe, na huitafakari sheria yake mchana na usiku.

3Atakuwa kama mti uliopandwa karibu na mkondo wa maji ambao huzaa matunda yake kwa majira yake, ambao majani yake hayakauki; lolote afanyalo litafanikiwa.

4Waovu hawako hivyo, wao badala yake ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

5Kwa hivyo waovu hawatasimama katika hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.

6Kwa kuwa Yahweh huikubali njia ya wenye haki, njia ya waovu itaangamizwa.

Soma sura nzima: Zaburi 1

Kwa Kiingereza

Berean Standard BiblePsalm 1Blessed is the man who does not walk in the counsel of the wicked, or set foot on the path of sinners, or sit in the seat of mockers. But his delight is in the Law of the LORD, and on His law he meditates day and night. He is like a tree planted by streams of water, yielding its fruit in season, whose leaf does not wither, and who prospers in all he does. Not so the wicked! For they are like chaff driven off by the wind. Therefore the wicked will not stand in the judgment, nor sinners in the assembly of the righteous. For the LORD guards the path of the righteous, but the way of the wicked will perish.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Zab 26:4–5Mimi sichangamani na watu waovu, wala sichangamani na watu wanafiki. Ninachukia waovu, na siishi na waovu.
Mit 4:14–15Usifuate njia ya waovu wala usiende katika njia ya watendao uovu. Jiepushe nayo, usipite katika njia hiyo; geuka na upite njia nyingine.
Yer 17:8Kwa maana atakuwa kama mmea karibu na maji kando ya mto; mizizi yake itaenea. Hawezi kuona joto likija, kwa kuwa majani yake yatakuwa mabichi. Kisha mwaka wa ukame hawezi kuwa na wasiwasi, wala hataacha kuzalisha matunda.
Mit 13:20Tembea pamoja na watu wenye hekima nawe utakuwa na hekima, bali rafiki wa wapumbavu atateseka.
Zab 119:1–2Wamebarikiwa wale ambao njia zao hazina lawama, waenendao katika sheria ya Yahwe. Wamebarikiwa wale wazishikao amri zake thabiti, wamtafutao kwa moyo wao wote.
Yer 15:17Sikuketi katika mkutano wa wale waliosherehekea au waliofurahi. Nimeketi kwa faragha kwa sababu ya mkono wako wenye nguvu, kwa maana umenijaza na hasira.
Mt 7:13–14Ingieni kwa kupitia geti jembamba. Kwa kuwa geti ni pana na njia ni pana inayoongoza kwenye uharibifu, na kuna watu wengi wanaopitia njia hiyo. Geti ni jembamba, Geti jembamba ni njia inayongooza katika uzima na ni wachache wanaoweza kuiona.
Lk 11:28Lakini yeye akasema, wamebarikiwa wale wasikio neno la Mungu na kulitunza.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki