Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Zaburi 34:17–20
Mstari wa Biblia · ULB
Zaburi 34:17–20
17Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote.
18Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.
19Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote.
20Yeye huitunza mifupa yake yote, hakuna hata mmoja wao utavunjika.
Katika muktadha
14Uache uovu na utende mema. Uitafute amani na kuiendea amani.
15Macho ya Yahwe yako kwenye haki na masikio yake huelekea kulia kwao.
16Uso wa Yahwe uko kinyume na wale watendao uovu, kuikatilia mbali kumbukumbu yao duniani.
17Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote.
18Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.
19Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote.
20Yeye huitunza mifupa yake yote, hakuna hata mmoja wao utavunjika.
21Uovu utawauwa waovu. Wale wachukiao haki watahukumiwa.
22Yahwe huokoa maisha ya watumishi wake. Hakuna atakaye hukumiwa hata mmoja atafutaye usalama katika yeye.
Kwa Kiingereza
The righteous cry out, and the LORD hears; He delivers them from all their troubles. The LORD is near to the brokenhearted; He saves the contrite in spirit. Many are the afflictions of the righteous, but the LORD delivers him from them all. He protects all his bones; not one of them will be broken.Imenukuliwa katika Agano Jipya
Mambo haya yalikuwa ili lile neno lililonenwa lipate kutimia, “Hakuna hata wake mmoja utakaovunjwa.”Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
Huponya mioyo iliyopondeka na kuganga majeraha yao.Yahwe yu karibu na wote wamwitao, wale wamwitao yeye katika uaminifu.Maana yeye allye juu palipoinuka, anayeishi katika uzima wa milele, ambaye jina lake ni mtakatifu, asema hivi, ''Ninaishi mahali pa juu na mahali patakatifu pamoja na yeye pia aliyemnyenyekevu na moyo uliopondeka, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu na kufufua mioyo ya wanaojutia.Roho ya Bwana Yahwe i juu yangu, maana Yahwe amenipaka mafuta mimi kuhiubiri habari njema kwa wenye taabu. Amenituma mimi kuwaponywa waliopondeka mioyo, kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kufungua gereza ili waliofungwa waweze kutoka.Sadaka ya Mungu ni roho iliyovunjika. Wewe, Mungu hautadharau moyo uliopondeka na kujutia.Wapendwa, msihesabu jaribu ambalo huja kuwajaribu kama kitu kigeni, ingawa kuna kitu kigeni kilichokuwa kinatukia kwenu. Lakini kwa kadri mnavyozidi kupata uzoefu wa mateso ya Kristo, furahini, ili kwamba mfurahi pia na kushangilia katika ufunuo wa utukufu wake.Nitawapatia moyo mpya na roho mpya sehemu zenu za ndani, na nitautoa moyo wa jiwe kutoka kwenye nyama zenu. Kwa kuwa nitawapatia moyo wa nyama.Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote.Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki