Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › 2 Wathesalonike 3:10

Mstari wa Biblia · ULB

2 Wathesalonike 3:10

Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, “Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile.”

Soma sura nzima: 2 Wathesalonike 3

Katika muktadha

7Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ni sawa kwenu kutuiga sisi. Hatukuishi miongoni mwenu kama wale ambao hawakuwa na nidhamu.

8Na hatukula chakula cha mtu yeyote bila kukilipia. Badala yake, tulifanya kazi usiku na mchana kwa kazi ngumu na kwa shida, ili tusiweze kuwa mzigo kwa yeyote katika ninyi.

9Tulifanya hivi si kwa sababu hatuna mamlaka. Badala yake, tulifanya hivi ili tuwe mfano kwenu, ili kwamba mweze kutuiga sisi.

10Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, “Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile.”

11Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi wanaenenda kwa uvivu miongoni mwenu. Hawafanyi kazi lakini badala yake ni watu wasio na utaratibu.

12Sasa hao nao tunaagiza na kuwaasa katika Bwana Yesu Kristo, kwamba lazima wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.

13Lakini ninyi, ndugu, msizimie roho katika kufanya yaliyo sahihi.

2 Wathesalonike 3

Kwa Kiingereza

Berean Standard Bible2 Thessalonians 3:10For even while we were with you, we gave you this command: “If anyone is unwilling to work, he shall not eat.”

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Mwa 3:19Kwa jasho la uso wako utakula mkate, mpaka utakapo irudia ardhi, ambayo kwayo ulitwaliwa. kwa kuwa wewe ni mavumbi na kwenye mavumbi utarudi.”
1 The 4:11Twawasihi mtamani kuishi maisha ya utulivu, kujali shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu, kama tulivyowaamuru.
Mit 13:4Hamu ya watu wavivu ni uchu lakini hawapati kitu, bali hamu ya watu wenye bidii hutoshelezwa sana.
Mit 20:4Mtu mvivu halimi majira ya kipupwe; hutafuta mazao wakati wa mavuno lakini hapati kitu.
Mit 21:25Shauku ya mtu mvivu itamuua, maana mikono yake hukataa kufanya kazi.
Mit 24:30–34Nilikwenda jirani na shamba la mtu mvivu, nikapita kwenye shamba la mzabibu la mtu asiye na akili. Miiba imeota kila sehemu, ardhi ilikuwa imefunikwa kwa upupu, na ukuta wake wa mawe ulikuwa umebomoka. Kisha nikaliona na kufikiria juu yake; nikatazama na kupokea mafundisho. Kulala kidogo, kusinzia kidogo, kupumzika kwa kukunja mikono kidogo- na umasikini huja kwa kutembea juu yako, na mahitaji yako kama askari mwenye silaha.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki