29Wakati wakitoka Yeriko, umati mkubwa ulimfuata.
30Na waliwaona vipofu wawili wameketi kando ya barabara. Waliposikia kuwa Yesu alikuwa anapita, walipaza sauti na kusema, “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie.”
31Lakini umati ukawakemea, na kuwaambia nyamazeni. Hata hivyo, wao wakapaza sauti zaidi na kusema, “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie.”
32Kisha Yesu alisimama na aliwaita na kuwauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”
33Wakamwambia, “Bwana kwamba macho yetu yafumbuliwe.”
34Basi Yesu, akiwa amevutwa na huruma, akayagusa macho yao, mara hiyo, wakapokea uwezo wa kuona na wakamfuata.