Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Katika Yerusalemu

Injili kando kwa kando · Katika Yerusalemu

Kuingia Yerusalemu

Mt 21:1–11 · Mk 11:1–11 · Lk 19:28–40 · Yn 12:12–19

Mathayo

Mt 21:1–11

1Yesu na wanafunzi wake wakafika karibu na Jerusalemu na wakaenda mpaka Bethfage, katika mlima mizeituni, kisha Yesu akawatuma wanafunzi wawili,

2akiwaambia, “Nendeni katika kijiji kinachofuata, na mara moja mtamkuta punda amefungwa pale, na mwanapunda pamoja naye. wafungueni na kuwaleta kwangu.

3Ikiwa mtu yeyote akiwaambia chochote kuhusu hilo, mtasema, 'Bwana anawahitaji, ' na mtu huyo mara moja atawaruhusu mje pamoja nao”

4Jambo hili lilitokea ni lile lililosemwa kupitia kwa nabii lazima litimizwe. Akawaambia,

5Waambie binti Sayuni, tazama, mfalme wako anakuja kwenu, mnyenyekevu na akiwa amempanda punda, na mwana punda mme, mwana punda mchanga.

6Kisha wanafunzi waliondoka na kufanya kama Yesu alivyowaagiza.

7Wakamleta punda na mwanapunda, na kuweka nguo zao juu yao, naye Yesu akakaa pale.

8Wengi katika mkusanyiko walitandaza nguo zao njiani, na wengine walikata matawi kutoka kwenye miti na kutandaza barabarani.

9Umati uliomtangulia Yesu na wale waliomfuata walipaza sauti, wakisema,”Hosana kwa mwana wa Daudi! Ni mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana. Hosana juu zaidi!”

10Yesu alipofika Yerusalemu, mji mzima ulishtuka na kusema, “Huyu ni nani?

11“Umati ulijibu, “Huyu ni Yesu Nabii, kutoka Nazareti ya Galilaya.”

Marko

Mk 11:1–11

1Wakati huo walipokuja Yerusalemu, walipokaribia Besthfage na Bethania, katika Mlima wa Mizeituni, Yesu aliwatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake

2na aliwaambia, “Nendeni katika kijiji kinachokabiliana nasi. Mara mtakapoingia humo, mtamkuta mwanapunda ambaye hajapandwa. Mfungueni na mmlete kwangu.

3Na kama yeyote akiwaambia, 'Kwa nini mnafanya hivi'?, mnapaswa kusema, 'Bwana anamhitaji na mara atamrudisha hapa'.”

4Walikwenda na kumkuta mwanapunda amefungwa nje mlangoni kwenye mtaa ulio wazi, nao walimfungua.

5Na baadhi ya watu walikuwa wamesimama pale na waliwaambia, “Mnafanya nini, kumfungua mwanapunda huyo?”

6Waliwaambia kama Yesu alivyowaambia, na watu wakawaacha waende.

7Wanafunzi wawili walimleta mwanapunda kwa Yesu na walitandika mavazi yao juu yake ili Yesu aweze kumpanda.

8Watu wengi wakatandika mavazi yao barabarani, na wengine wakatandika matawi waliyoyakata kutoka mashambani.

9Wale waliokwenda mbele yake na wale waliomfuata walipiga kelele, “Hosana! Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana.

10Ubarikiwe ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi! Hosana kwa aliye juu”

11Ndipo Yesu aliingia Yerusalemu na alikwenda hekaluni na alitazama kila kitu. Sasa, wakati ulikuwa umeenda, alikwenda Bethania pamoja nao kumi na wawili.

Luka

Lk 19:28–40

28Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.

29Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,

30akisema: 'Nendeni katika kijiji cha jirani. Mkiingia, mtakuta mwana-punda hajapandwa bado. Mfungueni, mkamlete kwangu.

31Kama mtu akiwauliza, 'Mbona mnamfungua? ' Semeni, “Bwana anamhitaji. ''

32Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia.

33Walipokuwa wanamfungua mwana punda wamiliki wakawaambia, 'Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?'

34Wakasema, 'Bwana anamhitaji. '

35Basi, wakampelekea Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana punda na wakampandisha Yesu juu yake.

36Alipokuwa akienda watu wakatandaza mavazi yao barabarani.

37Alipokuwa anateremka mlima wa Mizeituni, jumuiya yote ya wanafunzi wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona,

38wakisema, 'Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana! Amani mbinguni, na utukufu juu!'

39Baadhi ya Mafarisayo katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako. '

40Yesu akajibu, akasema, 'Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapaza sauti. '

Yohana

Yn 12:12–19

12Na siku ya pili yake umati mkubwa walikuja kwenye sikukuu. Waliposikia ya kuwa Yesu anakuja Yerusalemu,

13walichukua matawi ya miti ya mitende na kutoka nje kwenda kumlaki na wakapiga kelele, “Hosana! Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli.”

14Yesu alimpata mwana-punda akampanda; kama vile ilivyoandikwa,

15“Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda.”

16Wanafunzi wake hawakuyaelewa mambo haya hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kuwa mambo haya aliandikiwa yeye na ya kwamba wametenda mambo haya kwake.

17Basi lile kundi la watu waliokuwepo pamoja na Yesu wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, wakashuhudia kwa wengine.

18Na ilikuwa kwa sababu hii pia kwamba kundi la watu walikwenda kumlaki kwasababu walisikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo.

19Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, “Tazama, sasa hamwezi kufanya lolote; tazama, ulimwengu umekwenda kwake.”

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY