Gundua › Injili kando kwa kando › Katika Yerusalemu
Injili kando kwa kando · Katika Yerusalemu
Funzo la mtini
Mt 24:32–35 · Mk 13:28–31 · Lk 21:29–33
Mt 24:32–3532Jifunzeni somo kutokana na mti mtini. Mara tu tawi linapochipuka na kutoa majani, mnajua kwamba kiangazi kinakaribia.
33Hivyo pia, mtakapoona mambo haya yote, mnapaswa kujua kwamba amekaribia, karibu na malango.
34Kweli nawaambia, kizazi hiki hakitapita, hadi mambo yote haya yatakuwa yametokea.
35Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Mk 13:28–3128Kwa mtini jifunzeni. Kama tawi liwezavyo kutoa na kuweka haraka majani yake, ndipo mtajua kwamba kiangazi kiko karibu.
29Ndivyo ilivyo, mtakapoona mambo haya yakitokea, jueni kwamba yuko karibu, na malango.
30Kweli, nawambieni, hiki kizazi hakitapita mbali kabla mambo haya hayajatokea.
31Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Lk 21:29–3329Yesu akawaambia kwa mfano, “Uangalieni mtini, na miti yote.
30Inapotoa machipukizi, mnajionea wenyewe na kutambua kwamba kiangazi tayari kiko karibu.
31Vivyo hivyo, mnapoona mambo haya yanatokea, ninyi tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu umekaribia.
32Kweli, nawaambieni, kizazi hiki hakitapita, mpaka mambo haya yote yatakapotokea.
33Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY