Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Hatia na aibu

Hisia

Biblia inasema nini kuhusu Hatia na aibu

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (13), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

1 Yoh 1:9Lakini tukizitubu dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
Rum 8:1Kwa hiyo basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Isa 54:4Usiogope maana hautahaibika, wala kukatishwa tamaa maana hautapatwa na aibu; hutasahau aibu ya ujana wako na aibu ya kutelekezwa.
Rum 3:23Kwa kuwa wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
Isa 61:7Badala yake aibu yenu itaongezeka; na badala ya fedhea walifurahia juu ya sehemu yao. Hivyo basi sehemu yao itaongezeka mara mbili katika nchi na furaha ya milele itakuwa yao.
1 Yoh 2:1Watoto wangu wapendwa, nawaandikia mambo haya kwenu ili msitende dhambi. Lakini kama mmoja wenu akitenda dhambi, tunaye wakili aliye pamoja na Baba, Yesu Kristo- ambaye ni mwenye haki.
Zab 34:4–5Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote. Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu.
Ebr 12:2Tuyaelekeze macho yetu kwa Yesu, aliye mwanzilishi na mwenye kutimiliza imani yetu, ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahmili msalaba, akiidharau aibu yake, na akakaa chini mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
Rum 10:11Kwa kuwa andiko lasema, “Kila amwaminiye hata aibika.”
Rum 5:1Kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa njia ya imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Mik 7:19Tena utakuwa na huruma juu yetu; utayakanyaga maovu chini ya miguu yako. Utazitupa dhambi zetu zote kwenye vilindi vya bahari.
Mdo 8:22Hivyo basi tubu maovu yako na kumwomba Mungu labda utasamehewe fikra za moyo wako.
Lk 15:7nawaambia vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, zaidi ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0