Mwanzo › Biblia inasema nini › Wasiwasi na hangaiko
Hisia
Biblia inasema nini kuhusu Wasiwasi na hangaiko
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Flp 4:6–7
Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali, kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu. Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaad Kristo Yesu.1 Pet 5:7
Mwekeeni fadhaa zenu juu yake, kwa sababu anawajali.Yn 14:27
Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msiifanye mioyo yenu kuwa na mahangaiko, na woga.Isa 41:10
Usiogope maana mimi niko pamoja na wewe. Usiwe na wasiwasi, maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, na nitakusaidia, wewe, na Nitakushika kwa mkono wa haki yangu.Mt 6:34
Kwa hiyo, usione shaka kwa ajili ya kesho, kwa kuwa kesho itajishughulikia yenyewe. Kila siku inatosha kuwa na tatizo lake yenyewe.Mit 12:25
Mashaka katika moyo wa mtu humwelemea, bali neno zuri humfurahisha.2 Tim 1:7
Kwa kuwa Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na upendo na nidhamu.Zab 56:3
Wakati nina woga, nitaweka imani yangu katika wewe.Zab 55:22
Umtwike mizigo yako Yahwe, naye atakusaidia; yeye hataruhusu mtu mwenye haki kuyumbayumba.Zab 94:19
Wasiwasi uwapo mwingi ndani yangu, faraja yako hunifurahisha.Mt 11:28–30
Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.Flp 4:13
Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.Zab 34:4
Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote.Yos 1:9
Je si mimi niliyekuagiza? Uwe hadori na jasiri! Usiogope. Usivunjike moyo. Yahweh Mungu wako yuko pamoja nawe kila uendeko.Isa 35:4
Waambie wenye moyo wa uwoga, ''Wawe imara, wasiogope! Tazama, Mungu wako anakuja na kisasi, kwa ajili ya malipo ya Mungu. Atakuja na kutuokoa.''Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0