Mwanzo › Biblia inasema nini › Furaha
Hisia
Biblia inasema nini kuhusu Furaha
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (14), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Flp 4:4
katika Bwana siku zote. tena nitasema, furahini.Zab 144:15
Wamebarikiwa watu wenye baraka hizo; furaha ina watu ambao Mungu wao ni Yahwe.Mit 15:13
Moyo wenye furaha husababisha uchangamfu wa uso, bali huzuni huvunja moyo.Mit 17:22
Moyo mchangamfu ni dawa njema, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.Zab 37:4
Kisha ufurahi mwenyewe katika Yahwe, naye atakupa matamanio ya moyo wako.Mhu 3:12–13
Ninajua kuwa hakuna kilicho bora kwa mtu yeyote kuliko kufurahi na kutenda mema maadamu anaishi- na kwamba kila mmoja anapaswa ale na kunywa na anapaswa kuelewa jinsi ya kufurahia mazuri ambayo yanatoka katika kazi zake zote. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.Rum 15:13
Sasa Mungu wa tumaini awajaze na furaha yote na amani kwa kuamini, ili kwamba muweze kuzidi katika tumaini, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.Rum 12:12
Furahini katika ujasiri mlionao kuhusu siku zijazo. Muwe na subira katika matatizo yenu. Mdumu katika kuomba.Zab 16:11
Wewe hunifundisha njia ya maisha; furaha tele inakaa katika uwepo wako; furaha inakaa katika mkono wako wa kuume milele!”Yn 16:24
Mpaka sasa hamjaomba lolote kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapokea ili kwamba furaha yenu ikamilike.Gal 5:22–23
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani, upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo.Zab 34:8
Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.Isa 26:3–4
Akili mlionayo, mtamuhifadhi yeye katika amani kamili, maana anawamini ninyi. Mwamini Yahwe daima; maana Yaha, Yahwe, ni mwamba wa milele.Yer 29:11
Kwa maana mimi mwenyewe naijua mipangao niliyonayo kwa ajili yenu—hili ni tangazo la Yahwe—mipango kwa ajili ya amani na siyo kwa ajili ya mabaya, ili kuwapa ninyi tumaini na siku zenu za mwisho.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0