Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Kuridhika

Hisia

Biblia inasema nini kuhusu Kuridhika

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Flp 4:11–13Sisemi hivyo ili kujipatia kitu kwa ajili ya mahitaji yangu. Kwani nimejifunza kuridhika katika hali zote. Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa na pia katika hali ya kuwa na vingi. Katika mazingira yote haya mimi nimejifunza siri ya namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhihtaji. Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.
1 Tim 6:6–8Sasa utauwa na kuridhika ni faida kubwa. Kwa maana hatukuja na chochote duniani. Wala hatuwezi kuchukua chochote kutoka duniani. Badala yake, tutosheke na chakula na mavazi.
Ebr 13:5Basi njia zenu za maisha ziwe huru katika upendo wa pesa. Muwe wanoridhika na vitu mulivyonavyo, kwani Mungu mwenyewe alisema, “Sitawaacha ninyi kamwe, wala kuwatelekeza ninyi.”
Mt 6:31–33Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, 'Je tutakula nini?' au “Je tutakunywa nini?” au “Je tutavaa nguo gani?” Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo. Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako.
Lk 12:15Ndipo akawaambia, Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo.”
2 Kor 12:10Kwa hiyo ninatosheka kwa ajili ya Kristo, katika udhaifu, katika matukano, katika shida, katika mateso, katika hali ya masikitiko. Kwa kuwa wakati nikiwa dhaifu, kisha nina nguvu.
Flp 4:19Kwa ajili hiyo, Mungu wangu atawajazeni mahitaji yenu kwa utajiri wa utukufu wake katikaYesu Kristo.
Mt 6:25Kwa hiyo nakuambia, usiwe na mashaka kuhusu maisha yako, kuwa utakula nini au utakunywa nini, au kuhusu mwili wako, utavaa nini. Je! Maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi?
Mit 16:8Bora kitu kidogo pamoja na haki, kuliko mapato makubwa pamoja na udhalimu.
Mhu 5:12Usingizi wa mfanyakazi ni mtamu, kama anakula kidogo au sana, lakini utajiri wa mtu tajiri haumuruhusu yeye kulala vizuri.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0