Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Huzuni na sonona

Hisia

Biblia inasema nini kuhusu Huzuni na sonona

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Ikiwa ni vigumu sana, usibaki peke yako na jambo hili: zungumza na mtu unayemwamini, padri au mchungaji, au daktari.

Zab 34:18Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.
Yak 1:2–4Hesabuni kuwa ni furaha zaidi, ndugu zangu, mnapopita katika matatizo mbali mbali, mkijua kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huwapa uvumilivu. Acheni uvumilivu uikamilishe kazi yake, kwamba muweze kukomaa kikamilifu, bila kupungukiwa katika lolote.
Flp 4:7Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaad Kristo Yesu.
Yak 5:13Kuna yeyote miongoni mwenu ana mateso? Lazima aombe. Je, mtu yeyote ni mwenye kuchangamka? Na aimbe sifa.
Mt 5:4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
Ufu 21:4Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na hapatakuwa na kifo tena, au kuomboleza, au kulia, au maumivu. Mambo ya zamani yamekwishakupita.
2 Kor 7:6Lakini Mungu, anayefariji waliokata tamaa, alitufariji kwa ujio wa Tito.
Zab 30:5Kwa kuwa hasira yake ni ya muda tu; bali neema yake yadumu milele. Kilio huja usiku, bali furaha huja asubuhi.
Zab 55:22Umtwike mizigo yako Yahwe, naye atakusaidia; yeye hataruhusu mtu mwenye haki kuyumbayumba.
Mit 12:25Mashaka katika moyo wa mtu humwelemea, bali neno zuri humfurahisha.
Yn 14:1“Usiruhusu moyo wako kuwa katika mahangaiko. Unamwamini Mungu niamini pia na mimi.
2 Kor 1:3–4Na asifiwe Mungu na Baba wa Bwana Yesu Kristo. Yeye ni Baba wa rehema na Mungu wa faraja yote. Mungu hutufariji sisi katika mateso yetu yote, ili kwamba tuweze kuwafariji wale walio katika mateso. Tunawafariji wengine kwa faraja ileile ambayo Mungu alitumia kutufariji sisi.
Zab 147:3Huponya mioyo iliyopondeka na kuganga majeraha yao.
Zab 23:4Hata ijapokuwa nikipita katika bonde la uvuli na giza nene, sitaogopa kudhurika kwa kuwa wewe uko pamoja nami; fimbo yako na gongo lako vya nifariji.
2 Kor 12:9Naye akaniambia, “Neema yangu inatosha kwa ajili yako, kwa kuwa nguvu hufanywa kamili katika udhaifu. Hivyo, ningetamani zaidi kujivuna zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili kwamba uwezo wa Kristo uweze kukaa juu yangu.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0