Mwanzo › Biblia inasema nini › Hofu
Hisia
Biblia inasema nini kuhusu Hofu
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (14), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
2 Tim 1:7
Kwa kuwa Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na upendo na nidhamu.Yos 1:9
Je si mimi niliyekuagiza? Uwe hadori na jasiri! Usiogope. Usivunjike moyo. Yahweh Mungu wako yuko pamoja nawe kila uendeko.1 Yoh 4:18
Hakuna hofu ndani ya pendo. Lakini pendo kamili huitupa hofu nje, kwa sababu hofu huhusiana na hukumu. Lakini yeye aogopaye hajakamilishwa katika pendo.Isa 41:10
Usiogope maana mimi niko pamoja na wewe. Usiwe na wasiwasi, maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, na nitakusaidia, wewe, na Nitakushika kwa mkono wa haki yangu.Zab 23:4
Hata ijapokuwa nikipita katika bonde la uvuli na giza nene, sitaogopa kudhurika kwa kuwa wewe uko pamoja nami; fimbo yako na gongo lako vya nifariji.Ebr 13:6
Basi tulidhikeni ili tusema kwa ujasiri, “Bawa ni msaidizi wangu; Sitaogopa. Mwanadamu aweza kunifanya nini?”Zab 34:4
Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote.Zab 27:1
Zaburi ya Daudi. Yahwe ni nuru yangu na wokovu wangu; nimuogope nani? Yahwe ni salama ya maisha yangu; ni mhofu nani?Yn 14:27
Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msiifanye mioyo yenu kuwa na mahangaiko, na woga.Rum 8:15
Kwa kuwa hamkupokea roho wa utumwa tena hata muogope. Badala yake, mlipokea roho ya kufanywa kuwa wana, ambayo kwayo tunalia, “Abba, Baba!”Kum 31:8
Yahwe, yeye ndiye atakwenda kabla yako; atakuwa pamoja nawe; hatakuangusha wala hatakutelekeza; usiogope, usivunjike moyo.”Mt 8:24–26
Tazama, ikainuka dhoruba kuu juu ya bahari, kiasi kwamba mtumbwi ulifunikwa na mawimbi. Lakini Yesu alikuwa amelala. Wanafunzi wakaja kwake na kumwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe sisi, tunaelekea kufa!” Yesu akawaambia, “kwa nini mnaogopa, ninyi wenye imani ndogo?” Ndipo akaamka na kuukemea upepo na bahari. Kisha kukawa na utulivu mkuu,Mit 29:25
Kumwogopa binadamu ni mtego, bali mwenye kumtumaini Yehova atalindwa.Zab 56:3–4
Wakati nina woga, nitaweka imani yangu katika wewe. Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu - nimeweka imani yangu katika Mungu; sitaogopa; mtu wa kawaida atanifanya nini?Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0