Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Hasira

Hisia

Biblia inasema nini kuhusu Hasira

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Yak 1:19–20Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika, kwa kuwa hasira ya mwanadamu haiwezi kutenda haki ya Mungu.
Efe 4:26–27Mwe na hasira, lakini msitende dhambi.” Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu. Msimpe Ibilisi nafasi.
Mit 15:1Jawabu la upole huondoa ghadhabu, bali neno la ukatili huchochea hasira.
Mit 14:29Mtu mvumilivu anaufahamu mkubwa, bali mtu mwepesi wa kuhamaki hukuza upuuzi.
Efe 4:31Lazima muweke mbali uchungu wote, ghadhabu, hasira, ugomvi, na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wema ninyi kwa ninyi.
Mit 19:11Busara humfanya mtu achelewe kukasirika na utukufu wake ni kusamehe kosa.
Mit 29:11Mpumabavu huonyesha hasira yake, bali mtu mwenye busara huishikilia na kujituliza mwenyewe.
Mit 16:32Ni bora kukawia kuwa na hasira kuliko kuwa shujaa na mwenye kutawala roho yake ni imara zaidi kuliko yule anayeuteka mji.
Zab 37:8Usikasilile na kugadhabika. Usiogope. Hii huleta matatizo tu.
Mhu 7:9Usikasirike haraka rohoni mwako, kwa sababu hasira hukaa katika mioyo ya wapumbavu.
Mit 15:18Mtu mwenye hasira huchochea mabishano, bali mtu ambaye hukawia kukasirika hutuliza ugomvi.
Kol 3:8Lakini sasa ni lazima myaondoe mambo haya yote. Yaani, ghadhabu, hasira, nia mbaya, matusi, na maneno machafu yatokayo vinywani mwenu.
Efe 4:32Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Mt 5:22Lakini nawaambia yeyote amchukiaye ndugu yake atakuwa katika hatari ya hukumu. Na yeyote amwambiaye ndugu yake kuwa, 'Wewe ni mtu usiyefaa!' atakuwa katika hatari ya baraza. Na yeyote asemaye, 'Wewe mjinga!' atakuwa katika hatari ya moto wa jehanamu.
Mit 14:17Yeye ambaye anakuwa na hasira kwa haraka hufanya mambo ya kipumbavu, na mtu anayefanya hila mbaya huchukiwa.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0