Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Wivu na husuda

Hisia

Biblia inasema nini kuhusu Wivu na husuda

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

Mit 14:30Moyo wenye raha ni uzima wa mwili, bali husuda huozesha mifupa.
Yak 3:16Kwa kuwa palipo na wivu na ubinafsi upo, kuna vurugu na kila matendo maovu
Mit 27:4Kuna ukatili wenye ghadhabu kali na mafuriko ya hasira, lakini ni nani anayeweza kusimama mbele ya wivu?
Gal 5:19–21Sasa matendo ya mwili yanaonekana. Nayo ni uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, husuda, kuwaka hasira, ushindani, faraka, mgawanyiko wa madhehebu, wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu.
1 Kor 3:3Kwa kuwa ninyi bado ni wa mwilini. Kwa kuwa wivu na majivuno yanaonekana miongoni mwenu. Je, hamuishi kulingana na mwili, na je, hamtembei kama kawaida ya kibinadamu?
1 Kor 13:4Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi
Yak 3:14Lakini kama mnao wivu mkali na nia ya ubinafsi mioyoni mwenu, msijivune na kusema uongo mkiupinga ukweli.
Kut 20:17Usitaman nyumba ya jirani yako; usitamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wakiume, mtumishi wake mwanamke, ng'ombe wake, punda wake, au chochote cha jirani yako.
Yak 4:2–3Mnatamani kile msichokuwa nacho. Mnauwa na mnafukuzia kile msichoweza kuwa nacho. Mnapigana na kugombana, na bado hampati kwa sababu hamumwombi Mungu. Mnaomba na hampokei kwa sababu mnaomba kwa ajili ya mambo mabaya, ili kwamba muweze kuvitumia kwa tamaa zenu mbaya.
Ayu 5:2Kwa kuwa hasira huua mtu mpumbavu; wivu huua mjinga.
Mhu 4:4Kisha nikaona kwamba kila tendo la kazi na kila kazi ya utashi ikawa wivu wa jirani ya mtu. Huu pia ni mvuke na kujaribu kuchunga upepo.
Mit 23:17Usiruhusu moyo wako kuwahusudu wenye dhambi, lakini endelea kumcha Yehova siku zote.
Mdo 7:9Mababu zetu wakamwonea wivu Yusufu wakamuuza katika nchi ya Misri, na Mungu alikuwa pamoja naye,
Gal 5:26Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu.
1 Pet 2:1Kwa hiyo wekeni pembeni uovu wote, udanganyifu, unafiki, wivu na kashifa.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0