Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 16 Mei
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 16 Mei 2027
Jumapili · Juma la 7 la Pasaka
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya Pentekoste
Sherehe · Rangi ya liturujia: nyekundu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Ilipofika siku ya Pentekoste, wote walikuwa pamoja sehemu moja. 2Ghafla ikatokea muungurumo kutoka mbinguni kama upepo mkali. ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 3Hapo zikawatokea ndimi, kama ndimi za moto zimegawanyika, zikawa juu yao kila mmoja wao. 4Wao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kusema kwa lugha zingine, kama vile Roho alivyowajalia kusema. 5Sasa walikuwapo wayahudi waliokuwa wanaishi Yerusalemu, wacha Mungu, kutoka kila taifa chini ya mbingu. 6Ngurumo hizi ziliposikiwa, kundi la watu likaja pamoja na wakiwa na wasiwasi kwa sababu kila mtu aliwasikia wakiongea kwa lugha yake mwenyewe. 7waliduwaa na kushangazwa, wao walisema, “Kweli, hawa wote wanaoongea siyo Wagalilaya? 8Kwa nini sisi tunawasikia, kila mmoja katika lugha tulizozaliwa nazo? 9Waparthia na Wamedi na Waelamu, na hao waishio Mesopotamia, Uyahudi, na Kapadokia, na katika Ponto na Asia, 10katika Frigia, Pamfilia, katika Misri, na sehemu ya Libya hata Kirene, na wageni kutoka Rumi, 11Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, tunawasikia wakizungumza katika lugha zetu kuhusu kazi za uweza wa Mungu.”
Wimbo wa katikati
1Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote, Ewe Yahwe Mungu wangu, wewe ni mkubwa sana; umevikwa kwa utukufu na enzi. 24Yahwe, ni jinsi gani kazi zako zilivyo nyingi na za aina mbalimbali! Kwa hekima ulizifanya zote; nchi inafurika kwa kazi zako. 29Unapouficha uso wako, wanateseka; ukiiondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini. 30Unapotuma Roho yako, wanaumbwa, nawe unaifanya upya nchi. 31Utukufu wa Yahwe na udumu milele; Yahwe na aufurahie uumbaji wake. 34Mawazo yangu na yawe matamu kwake; nitafurahia katika Yahwe.
Somo la pili
16Nasema, tembeeni kwa roho, na wala hamtazitimiza tamaa za mwili. 17Kwa kuwa mwili una tamaa kubwa dhidi ya Roho, na Roho ina tamaa kubwa dhidi ya mwili. Hizi zinapingana kila moja na nyingine. Matokeo ni kwamba hamfanyi vitu mnavyotamani kuvifanya. 18Lakini kama Roho anawaongoza ninyi, hamko chini ya sheria. 19Sasa matendo ya mwili yanaonekana. Nayo ni uasherati, uchafu, ufisadi, 20ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, husuda, kuwaka hasira, ushindani, faraka, mgawanyiko wa madhehebu, 21wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu. 22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani, 23upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo. 24Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya. 25Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho.
Injili
26Wakati mfariji amekuja, ambaye nitamtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyu ndiye, Roho wa kweli, ambaye anatokea kwa Baba, atanishuhudia. 27Ninyi pia mnanishuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo. 16:12Ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamtayaelewa sasa. 13Lakini, yeye, Roho wa kweli, akija, atawaongoza katika kweli yote; kwa kuwa hataongea kwa ajili yake mwenyewe; lakini yoyote atakayoyasikia, atayasema mambo hayo; na atayadhihirisha kwenu mambo yatakayokuja. 14Yeye atanitukuza mimi, kwa sababu atayachukua mambo yangu na atayatangaza kwenu. 15Vitu vyote alivyonavyo Baba ni vyangu; kwa hiyo, nimesema kwamba Roho atachukua mambo yangu na atayadhihirisha kwenu.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki