Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 20 Juni
Kalenda ya Kiorthodoksi · 7 Juni (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 20 Juni 2027
Jumapili · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Pentekoste Takatifu. Sikukuu ya Utatu Mtakatifu
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Sala ya Jioni: somo
16BWANA akamwambia Musa, “Niletee wazee sabini miongoni mwa Waisraeli. Hakikisha ni wazee na viongozi wa watu. Uwalete kwenye hema ya kukutania wasimame pamoja na wewe. 17Nami nitashuka niseme nawe mahali pale. Nitatoa sehemu ya roho iliyo ndani yako na kuwapatia wao. Nao watabeba mzigo wa watu pamoja nawe. na hautaubeba peke yako. 24Musa alitoka nje kwenda kuwaambia watu maneno ya BWANA. Aliwakusanya wazee sabini wa watu na kuwaweka kuizunguka hema. 25BWANA akashuka chini katika wingu akaongea na Musa. BWANA akachukua sehemu ya roho iliyokuwa kwa Musa na kuiweka kwa wale wazee sabini. Roho alipowashukia, wakaanza kutoa unabii, lakini ilitokea kwenye tukio hilo tu na haikujirudia tena. 26Watu wawili waitwao Elidadi na Medadi walibaki kambini. Lakini Roho aliwashukia pia. Majina yao yalikuwa yameandikwa kwenye orodha lakini walikuwa hawajaenda hemani. Hata hivyo nao walitoa unabii wakiwa kambini. 27Kijana mmoja huko kambini alikimbia akaenda kumwambia Musa, “Elidadi na Medadi wanatoa unabii kambini.” 28Joshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Musa, ambaye ni miongoni mwa wale aliowachagua akamwambia Musa, “Bwana wangu Musa, wazuie.” 29Musa akamwambia, “una wivu kwa niaba yangu? Natamani kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii na kwamba angeweka Roho yake juu yao wote!”
Sala ya Jioni: somo
23Furahini, enyi watu wa Sayuni, na kufurahi katika Bwana, Mungu wenu. Kwa maana atakupa mvua ya vuli kwa kiasi na kuleta mvua kwa ajili yenu, mvua ya vuli na mvua ya masika kama hapo awali. 24Sakafu ya kupepetea zitajaa ngano, na vyombo vitafurika kwa divai mpya na mafuta. 25“Nitawawezesha miaka ya mazao ambayo nzige walikula, Palale, nzige, na nzige wakuteketeza - jeshi langu lenye nguvu ambalo nimelituma kati yenu. 26Mutakula chakula tele na kushiba, na kulitukuza jina la Bwana, Mungu wenu, aliyefanya miujiza kati yenu, wala sitawaletea tena watu wangu. 27Utajua ya kwamba mimi niko kati ya Israeli, na kwamba mimi ni Bwana, Mungu wako, wala hakuna mwingine, wala sitawaletea aibu watu wangu. 28Itakuwa baada ya hayo nitamimina Roho yangu juu ya wenye mwili yote, na wana wenu na binti zenu watatabiri. Wazee wenu wataota ndoto, vijana wenu wataona maono. 29Pia juu ya watumishi na watumishi wa kike, siku hizo nitaimimina Roho wangu. 30Nitaonyesha maajabu mbinguni na duniani, damu, moto na nguzo za moshi. 31Jua litakuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla ya siku kuu na ya kutisha ya Bwana itakapokuja. 32Itakuwa kwamba kila mtu anayeita jina la Yahweh ataokolewa. Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na Yerusalemu watakuwa na wale waliokoka, kama Bwana alivyosema, na kati ya wale walisalia, wale ambao Bwana anawaita.
Sala ya Jioni: somo
24Nitawachukua kutoka mataifa na kuwakusanya kutoka kila nchi, na nitawaleta hata nchi yenu. 25Kisha nitanyunyiza maji masafi juu yenu ili muwe wasafi kutoka kwenye uchafu wote, na nitawasafisha kutoka sanamu zenu zenu. 26Nitawapatia moyo mpya na roho mpya sehemu zenu za ndani, na nitautoa moyo wa jiwe kutoka kwenye nyama zenu. Kwa kuwa nitawapatia moyo wa nyama. 27Nitaiweka Roho yangu ndani yenu na kuwawezesha kutembea katika sheria zangu na kuziweka hukumu zangu, hivyo mtazitenda. 28Kisha mtakaa katika nchi niliyowapa babu zenu; mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.
Sala ya Alfajiri: Injili
19Na ilipokuwa jioni, siku hiyo, siku ya kwanza ya juma, na milango ikiwa imefungwa mahali wanafunzi walipokuwapo kwa kuwahofia Wayahudi, Yesu alikuja na kusimama katikati yao na kuwaambia, “Amani iwe kwenu.” 20Alipokwisha sema haya akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Nao wanafunzi walipomwona Bwana walifurahi. 21Kisha Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama vile Baba alivyonituma mimi, vivyo hivyo nami nawatuma ninyi.” 22Yesu alipokwisha sema hayo, akawavuvia akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. 23Yeyote mmsameheye dhambi, wamesamehewa; na wale mtakaowafungia watafungiwa.”
Waraka
1Ilipofika siku ya Pentekoste, wote walikuwa pamoja sehemu moja. 2Ghafla ikatokea muungurumo kutoka mbinguni kama upepo mkali. ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 3Hapo zikawatokea ndimi, kama ndimi za moto zimegawanyika, zikawa juu yao kila mmoja wao. 4Wao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kusema kwa lugha zingine, kama vile Roho alivyowajalia kusema. 5Sasa walikuwapo wayahudi waliokuwa wanaishi Yerusalemu, wacha Mungu, kutoka kila taifa chini ya mbingu. 6Ngurumo hizi ziliposikiwa, kundi la watu likaja pamoja na wakiwa na wasiwasi kwa sababu kila mtu aliwasikia wakiongea kwa lugha yake mwenyewe. 7waliduwaa na kushangazwa, wao walisema, “Kweli, hawa wote wanaoongea siyo Wagalilaya? 8Kwa nini sisi tunawasikia, kila mmoja katika lugha tulizozaliwa nazo? 9Waparthia na Wamedi na Waelamu, na hao waishio Mesopotamia, Uyahudi, na Kapadokia, na katika Ponto na Asia, 10katika Frigia, Pamfilia, katika Misri, na sehemu ya Libya hata Kirene, na wageni kutoka Rumi, 11Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, tunawasikia wakizungumza katika lugha zetu kuhusu kazi za uweza wa Mungu.”
Injili
37Sasa katika siku ya mwisho, siku kubwa ya sikukuu, Yesu alisimama akapaza sauti, akisema, “Ikiwa yeyote ana kiu, na aje kwangu anywe. 38Yeye aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyosema, kutoka ndani yake itatiririka mito ya maji ya uzima.” 39Lakini aliyasema haya kuhusu Roho, ambaye wao wamwaminio watampokea; Roho alikuwa bado hajatolewa kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado. 40Baadhi ya makutano, waliposikia maneno haya, walisema, “Kweli huyu ni nabii.” 41Wengine walisema, “Huyu ni Kristo.” Lakini wengine walisema, “nini, Kristo aweza kutoka Galilaya? 42Maandiko hayajasema kuwa Kristo atatokea katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi alikuwa? 43Hivyo, pale ukainuka mgawanyiko katikati ya makutano kwa ajili yake. 44Wengine kati yao wangelimkamata, lakini hakuna aliyenyoosha mikono yake juu yake. 45Ndipo wale maofisa wakarudi kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, nao wakawaambia, “Kwa nini hamjamleta?” 46Maofisa wakajibu, “Hakuna mtu aliyewahi kuzungumza kama huyu kabla.” 47Ndipo Mafarisayo walipowajibu, “Na nyinyi pia mmepotoshwa? 48Kuna yeyote kati ya watawala anayemwamini, au yeyote wa Mafarisayo? 49Bali hawa makutano wasiojua sheria - wamelaaniwa.” 50Nikodemo akawaambia (yeye aliyemwendea Yesu zamani, akiwa mmoja wa Mafarisayo), 51“Je sheria yetu inamhukumu mtu isipokuwa amesikilizwa kwanza na kujua anachokifanya?” 52Walijibu na kumwambia, “Na wewe pia unatokea Galilaya? Tafuta na uone kwamba hakuna nabii aliyetokea Galilaya.” 8:12Tena Yesu akazungumza na watu akisema, “Mimi ni nuru ya ulimwengu; yeye anifuataye hatatembea gizani bali atakuwa na nuru ya uzima.”
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Theodoto wa Ankira, mwenye nyumba ya wageni (303)
- Wafiadini wa Kikasisi Androniko, Askofu Mkuu wa Perm, Aleksanda, Aleksi, Aleksanda, Valentino, Benyamini, Vikta, Aleksanda, Paulo, Vladimir, Ignatio, Leo, Mikaeli, Nikolao, Paulo, Aleksanda, Nikolao, mapadri, Gregori, shemasi, na Wafiadini Athanasio na Aleksanda (1918)
- Wafiadini wa Kikasisi Nikolao na Petro, mapadri (1919)
- Mfiadini wa Kikasisi Markelino, Papa wa Roma, na Wafiadini Klaudio, Kirino na Antonino (304)
- Mfiadini wa Kikasisi Markelo, Papa wa Roma, Wafiadini Sisinio na Kiriako, mashemasi, Smaragdo, Largio, Aproniano, Saturnino, Papio na Mauro, askari, na Kreskentiano, Wafiadini Priskila, Lukina na Artemia, binti wa mfalme (304-310)
- Wafiadini Kaleria (Valeria), Kiriakia na Maria huko Kaisaria ya Palestina (284–305)
- Mkutano wa Watakatifu wa Ivanovo
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 7 Juni katika kalenda ya kanisa ni 20 Juni katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki