32Yesu akawaita wanafunzi wake na kusema, “ Nimewaonea huruma umati, kwa sababu wamekuwa nami kwa siku tatu bila kula kitu chochote. Sitawaaga waende kwao bila kula, wasije wakazimia njiani.”
33Wanafunzi wake wakamwambia, “Ni wapi tunaweza kupata mikate ya kutosha hapa nyikani kushibisha umati mkuwbwa hivi?”
34Yesu akawaambia, “Mna mikate mingapi?” Wakasema, “Saba, na samaki wadogo wachache.”
35Yesu akawaamuru umati uketi chini.
36Aliitwaa ile mikate saba na samaki, na baada ya kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi. Wanafunzi wakawapa umati.
37Watu wote wakala na kutosheka. Na wakakusanya mabaki ya vipande vya chakula vilivyosalia vipande vipande, vilijaa vikapu saba.
38Wote waliokula walikuwa wanaume elfu nne bila wanawake na watoto.
39Kisha Yesu akauaga umati waende zao na akaingia ndani ya mashua na kwenda sehemu za Magadani.