21Ndipo Yesu akatoka mahali pale na akajitenga kuelekea pande za miji ya Tiro na Sidoni.
22Tazama akaja mwanamke Mkanani kutoka pande hizo. Akapaza sauti akisema, ''Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu anateswa sana na pepo.''
23Lakini Yesu hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakaja wakimsihi, wakisema, ''Muondoe aende zake, maana anatupigia kelele.''
24Yesu aliwajibu na kusema, Sikutumwa kwa mtu yeyoye isipokuwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.''
25Lakini alikuja na kuinama mbele yake, akisema, ''Bwana nisaidie.''
26Alimjibu na kusema, “Siyo vema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa,”
27Akasema, “Ndiyo, Bwana, hata hivyo mbwa wadogo hula chakula kiagukacho mezani mwa Bwana wao.”
28Ndipo Yesu akajibu na akisema “Mwanamke, imani yako ni kubwa. Na ifanyike kwako kama utakavyo.” Na binti yake alikuwa ameponywa katika wakati huo.